Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amebatilisha pendekezo la kufutwa shamba lenye ukubwa wa ekari 1,000 lililopo Kidunda wilayani Mvomero mkoani Morogoro linalomilikiwa na Rusimbi.
Uamuzi wa Dkt Mafuli kubatilisha ufutaji shamba hilo unatokana na kubainika kuwa pendekezo lililowasilishwa la kufutwa shamba hilo kwa madai ya kutoendelezwa kutokuwa za kweli na ulilenga kumdhulumu mmiliki wake.
Akitangaza uamuzi huo wa Raisi jana wilayani Mvomero, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema, baada ya kufuatilia mashamba yaliyopendekezwa kufutwa Dkt Magufuli alibaini taarifa alizopelekewa za kufuta shamba Cecilia hazikuwa sahihi na hivyo kuamua kubatilisha pendekezo lililowasilishwa kwake na kumpatia haki yake mmiliki.
Kufuatia hali hiyo Waziri Lukuvi aliwaonya maafisa ardhi nchini kuhakikisha wakati wa kufanya zoezi la ukaguzi/Upekuzi wa mashamba yasiyoendelezwa wanazingatia haki pamoja na kufuata sheria badala ya kufanya kazi hiyo kwa upendeleo au kumuonea mtu.
Kwa upande wake Cecilia George Rusimbi alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kubatilisha ufutaji sahamba lake na kuuelezea uamuzi huo kuwa umezingatia haki na kusikia kilio chake ambapo alisema umempa faraja baada ya kuhangaika sana kuhusiana na shamba hilo.
‘’Nimemiliki shamba tangu mwaka 1987 na kuhangaikia hati kwa muda mrefu na nimeshangazwa kuelezwa kuwa shamba langu liko katika mpango wa kufutwa kutokana na kutoendelezwa, hii imenifanya kuishi kwa wasiwasi’’ alisema Cecilia.
Waziri Lukuvi ameagiza shamba hilo la kilimo cha Michikichi, Mitiki na Bamboo kupangwa upya na mmiliki wake kupatiwa hati kulingana na upimaji utakaofanywa na kumtaka kuliendeleza kwa mujibu wa sheria.
Sambamba na sakata la shamba la Cecilia, Lukuvi aliagiza kupunguzwa ukubwa wa Shamba Sangasanga na Lubango lililodaiwa kuwa na ukubwa wa ekari 1,103 wakati uhalisia wa shamba hilo ni ekari 500 na kuagiza mmiliki wake kurudisha hati ili apatiwe hati ilinayolingana na uhalisia wake na ekari 603.5 zilizoongezwa zitabaki kuwa ardhi ya akiba.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇