Rais Dk. John Magufuli akimuapisha Balozi Maj. Jenerali Anselm Shigongo Bahati kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Misri, Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma, leo PICHA ZAIDI BOFYA HAPA |
Rais Dk. John Magufuli amewaapisha Mabalozi wapya watano aliowateua hivi karibuni na kuwataka kuripoti kwenye vituo vyao kazi kwenye nchi walizopangiwa katika kipindi kisichozidi wiki moja.
Hafla ya kuapishwa kwa Mabalozi hao imefanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, Mawaziri na Naibu Mawaziri, MakatibuWakuu, Viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, viongozi wa Dini, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Lameck Mlacha na viongozi wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa huo Dk. Binilith Mahenge.
Mabalozi walioapishwa na nchi walizopangiwa zikiwa kwenye mabano ni, Mej. Jen Anselm Shigongo Mlacha (Misri), Mohamed Abdallah Mtonga (Falme za Kiarabu), Dk. Jilly Elibariki Maleko (Burundi) Jestas Abouk Nyamanga (Ubelgiji) na Ali Jabir Mwadini (Saudi Arabia).
" Nawatakia heri katika majukumu yenu ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi nilizowapangia na mripoti katika vituo vyenu vipya vya kazi katika kipindi kisichozidi wiki moja" amesema Rais Dk. Magufuli wakati akizungumza baada ya kuwaapisha mabalozi hao.
Naye Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka Mabalozi hao pamoja na Mabalozi wengine wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kusimamia vizuri fedha na mali zilizopo katika Balozi hizo, na pia kusimamia vizuri utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ili Tanzania inufaike na uhusiano mzuri uliopo kati yake na nchi takazokuwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇