LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 26, 2019

NITAACHIA NGAZI MUHULA WANGU WA UONGOZI UKIMALIZIKA

Rais wa Nigeria ametoa matamshi hayo kufuatia kuenea tetesi katika mitandao ya kijamii kwamba, kuna mpango wa kubadilishwa katiba ili kumfungulia njia aweze kugombea katika muhula wa tatu.
Akizungumza katika mkutano wa chama chake tawala wa cha All Progressives Congress (APC) Rais Buhari amesema kuwa, hana mpango wa kubadilisha katiba na kuendelea kutawala nchini humo.
Rais Buhari amesisitiza kuwa, hana nia ya kufanya hivyo kama walivyofanya baadhi ya viongozi waliotawala nchi hiyo ambao waliondoa kipengee cha ukomo wa duru mbili za uongozi wa Rais ili waweze kugombea tena.
Rais Muhamadu Buhari na mpinzani wake Atiku Abubakar walipokuwa wakipiga kura katika uchaguzi uliopita
Habari ya kuweko juhudi za Rais Buhari kutaka kubadilisha kipengee cha ukomo wa uongozi wa duru mbili imeenea nchini Nigeria hasa katika mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanadai kuna mpango huo.
Hata hivyo Rais Buhari amekana hilo na kusistiza kuwa, ni tetesi ambazo hazina ukweli kwani binafsi hana mpango kama huo na akaeleza kwamba, ninafahamu vyema kwamba, huu ni muhula wangu wa mwisho wa uongozi na sina nia ya kutaka kusimama tena na kuomba kura za wananchi wa Nigeria.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages