LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 26, 2019

AWATAKA ASKARI ENEO LA MPAKANI KUJIWEKA TAYARI

Kiongozi huyo ametembelea eneo la Changrin lililo umbali wa kilometa 45 kutoka maeneo yanayodhibitiwa na nchi jirani ya Korea Kusini. Katika ziara hiyo Kim Jong-un amekitaka kikosi cha askari wanaolinda mpaka huo kuzidisha utayarifu wao kwa lengo la kukabiliana na vitisho vyovyote. Kadhalika amelitaka jeshi kufanya maneva mbalimbali za kijeshi ili kuinua uzoefu wa jeshi hilo.  Mwaka 2010 eneo la Changrin lilishuhudia mivutano kati ya nchi mbili hizo jirani. Aidha mwezi Machi mwaka huo meli moja ya kivita ya Korea Kusini ilizama baharini na kupelekea kufariki dunia watu 46 baada ya kukurubia eneo hilo la mpakani. Serikali ya Korea Kusini iliittuhumu Korea Kaskazini kuwa muhusika wa kuzama kwa meli yake hiyo ya kivita.
Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini akiwa eneo la Changrin
Hivi karibuni pia Kim Jong-un, Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini alilitaka jeshi la anga la nchi hiyo kujiweka tayari na kujizatiti kwa silaha ili kuwakabili maadui. Kim alitoa amri hiyo katika ufunguzi wa mazoezi ya jeshi la anga la Korea Kaskazini katika mji wa pwani wa Wonsan Kalma, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Kuvunjika mazungumzo kati ya Pyongyang na Washington kwa upande mmoja na kadhalika kati ya Pyongyang na Seoul kwa upande wa pili kunatajwa kuwa sababu ya kuongezeka mzozo katika eneo la Pwani ya Korea, huku Marekani ikitajwa kuwa muhusika mkuu wa hali hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages