Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC) Barnabas Mwakalukwa akitoa salama Jeshi
hilo jana wakati wa uzinduzi wa nyumba mpya za makazi mapya ya Askari
mjini Tabora.
Katibu
Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora (Serikali za Mitaa) Nathalis Linuma
akitoa salamu za Mkoa jana wakati wa sherehe fupi ya uzinduzi wa nyumba
mpya Askari mjini Tabora.
Baadhi ya Maaskati na Wageni waalikwa walioshiriki uzinduzi wa nyumba mpya za makazi ya askari jana mjini Tabora.Picha na Tiganya Vincent
………………..
NA TIGANYA VINCENT
MAJENGO
matatu ya makazi mapya ya Polisi yamegharimu jumla ya shilingi milioni
254 kukamilika zikiwemo zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na wadau Mkoani Tabora.
Akisoma
risala wakati wa uzinduzi wa majengo hayo Marakibu Mwandamizi wa Polisi
(SSP) Msabila Kulwa Bundala alisema kila jengo lina nyumba mbili za
makazi ambalo kila moja limegharimu shilingi milioni 84.6.
Alisema
katika kiasi cha fedha cha shilingi bilioni 10 , Mkoa wa Tabora ulipata
shilingi milioni 150 ambapo wadau wa Jeshi hilo walichangia zaidi ya
milioni 100.
Bundala alisema michango ya wadau ilijumuisha fedha tasimu , saruji , vifaa vya umeme na maji.
Naye
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora (Serikali za Mitaa) Nathalis
Linuma alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora kushirikiana na Jeshi la
Polisi katika kuboresha makazi ili wawe na mazingira mazuri ya kuishi
na kutoa huduma nzuri kwa jamii.
Alisema
maendeleo hayana mwisho ni vema utaratibu wa jamii kushirikiana na
Polisi kuboresha mazingira ya kuishi na kufanyia kazi yakaendelea ili
kuwawezesha kuishi sehemu moja ambayo itakuwa rahisi kuisaidia jamii
pindi wanapohitajika.
Kwa
upande wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Barnabas Mwakalukwa alitoa
wito kwa wadau mbalimbali Mkoani Tabora kusaidia kukamilisha majengo ya
Ofisi likiwemo la Asakari wa Usalama barabarani ambayo yalianza kujengwa
mwaka 2015 ambayo yamesimama.
Alisema
uwepo wa Ofisi ya za kutosha utaongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa
kuwa na mazingira mazuri ya kutoa huduma kwa wananchi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇