Kugunduliwa kwa
mafuta na gesi katika baadhi ya nchi za Afrika kumeweza kuokoa fedha
nyingi ambazo zingetumika kununua nishati nje kwa matumizi mbalimbali ya
maendeleo.
Kwa kipindi cha miaka 15, toka Tanzania ilipoanza
kuzalisha na kusambaza gesi, imeokoa kiasi cha shilingi Trilioni 30,
ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje kwa ajili ya kuzalisha umeme na
uendeshaji wa viwanda.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC James Mataragio, takriban asilimia 60 ya umeme unaozalishwa nchini unatumia gesi asilia, huku nishati hiyo pia ikitumika viwandani mbali na kutumika kuendesha magari katika siku za hivi karibuni.
- Jinsi kinyesi kinavyogeuka lulu Tanzania
- Tamko la mradi wa bomba la mafuta ghafi lasainiwa
- Rais Magufuli akutana na Dangote
Katika eneo la Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam, kunakopatikana kituo pekee kinachotumia mfumo wa gesi katika uendeshaji wa magari, Mwanahabari huyo alikutana na Augustin - dereva wa UBA, aalimwelezea ni nini haswa kilichomshinikiza kuanza kutumia mfumo wa gesi katika gari lake.
Dereva huyo anasema kwamba alilazimika kutumia nishati ya gesi kutokana na hali ngumu ya kiuchumi mbali na bei ya juu ya mafuta
''Ninatumia gesi kwa kuwa ni bei rahisi kulingana na hali ya uchumi ya sasa ilivyo, lakini pia ukitazama kuna tofauti kubwa sana ukilinganisha mafuta ambayo unaweza kutumia mengi kwa siku huku gesi ukitumia fedha chache lakini kwa muda mrefu''.
''Hii gesi nikijaza dola saba na Marekani in maana ninaweza kutembea kilomita 150 ukichanganya na foleni za mjini'', aliongezea.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC James Mataragio anasema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji vituo vingine viwili vikubwa vinatarajiwa kujengwa kwa ajili ya kusambaza gesi kwenye vituo vingine vidogo katika maeneo mbalimbali.
Bwana Mataragio anasema kwamba takriban magari 300 nchini Tanzania yamelkuwa yakitumia gesi badala ya mafuta , huku mengi zaidi yakiendelea kubadilishga mifumo yao ya mafuta hadi kuwa ile ya gesi
''Kufikia sasa zaidi ya magari 300 yanatumia gesi .Tulianza mwaka 2009 ambapo kituo cha kwanza cha gesi kilijengwa hapa Dar es salaam ambacho kinatumika katika kujaza magari gesi. Tangu kipindi hicho kumekuwa na karakarana ambazo zimekuwa zikibadilisha mifumo ya mafuta hadi gesi''.
Kupunguza gharama ya maisha
Uwepo wa gesi asilia inayozalishwa katika baadhi ya nchi za Afrika, sio tu utanufaisha mtu mmoja mmoja, kama ilivyo kwa Augustin dereva wa UBA nchini Tanzania kwa kupunguza gharama za uendeshaji wa gari, lakini pia kukua kwa uchumi wa nchi na maendeleo.Dokta Donald Mmari ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayojishughulisha na utafiti wa kupunguza umasikini REPOA
Anasema kwamba utumiaji wa gesi unaweza kuwa chanzo cha mapato makubwa ya taifa hilo ambacho lkinaweza kuimraisha poakubwa uchumi wa taifa hilo.
''Nchi nyengine tunaweza kuona kama vile China Malaysia na India magari yote ya kijamii yakiwemo mabasi yanatumia gesi asilia na kufanya gharama ya uchukuzi kushuka chini. Ni wakati tu kwamba tumeanza kuweka uwekezaji katika sekta hii''.
Aliongezea: Tuna nafasi kubwa kabisa ya kutumia gesi katika sekta nyengine sasa - hii pia inaweza kuwa chanzo cha kipato kikubwa katika matumizi ya serikali hususan katika kuwekeza katika miundo mbinu muhimu katika kuimarisha uchumi.
Mikataba na makampuni
Lakini hata hivyo, mafanikio haya yote ya kiuchumi yanayotokana na gesi asilia inayopatikana katika baadhi ya nchi za Afrika hayataweza kuwanufaisha wananchi kwa kiasi kikubwa iwapo mikataba inayoafikiwa na mataifa ama makampuni makubwa katika kusaidia upatikanaji wa gesi hiyo, itakuwa mibovu.Lulu Sailas Olang ni mtafiti kutoka Taasisi inayohusika na masuala ya utafiti ya kupunguza umasikini REPOA.
Anasema kwamba mataifa yanapaswa kuingia katika mikataba itakayoyawezesha kunufaika na rasilmali zake.
''Kabla ya kitu chochote ni muhimu kujua kwamba mikataba ni chombo muhimu kinachoamua ni kitu gani kitapatikana, na kitu cha kwanza tutakachokubaliana kati ya kampuni inayozalisha na serikali kwa niaba ya wananchi ni mkataba utakaoafikiwa baina ya pande hizo mbili. Iwapo mkataba huo utakuwa na vipengenele kandamizi mwisho wa siku hatutapata kile ambacho tulitarajia kukipata na manufaa yale yatakuwa magumu kuyaona hivyobasi ni muhimu kuingia katika mikataba baada ya kujua ina nini ndani yake na ni vitu gani vitapatikana''.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇