Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe Kisa Kasongwa akipokea msaada kwa ajili ya
waathirika wa maafa wilayani humo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya
Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, msaada huo umetolewa
na ofisi hiyo kupitia Mfuko wa maafa
Baadhi
ya wakazi wa kijiji cha Mapangoni kilichopo Kata ya Kerenge
wakishirikiana na wanajeshi kushusha baadhi ya vitu vya msaada
vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kupitia
Mfuko wa Maafa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kijijini hapo.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akipokea msaada kwa ajili ya waathirika
wa maafa mkoani humo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, msaada huo umetolewa na ofisi hiyo
kupitia Mfuko wa maafa.
Mkuu
wa wilaya ya Korogwe Kissa Kasongwa akisisitiza umuhimu wa kijiji hicho
kuhama katika eneo salama lilioainishwa na wilaya hiyo mara baada ya
kupokea msaada vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya
Waziri Mkuu, kupitia Mfuko wa Maafa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko
kijijini hapo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe,
akisisitiza umuhimu wa kijiji hicho kuhama katika eneo salama
lilioainishwa na wilaya hiyo mara baada ya kupokea msaada vilivyotolewa
Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Mfuko wa
Maafa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kijijini hapo
Baadhi
ya wananchi wa Kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge Wilayani Korogwe
wakifuatilia mkutano wa Mkuu wa wilaya hiyo Kissa Kasongwa na Mkurugenzi
wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe hawapo
pichani wakati walipopeleka misaada kwa waathirika wa maafa ya mafuriko
kutoka Ofisi ya waziri Mkuu, Mfuko wa maafa
************************************
Kamati
ya menejineti ya Maafa wilayani Korogwe imeelekezwa kutekeleza maazimio
ya Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge Wananchi wa
kijiji hicho chenye kaya zaidi ya 250 ambazo ziliridhia kuhama kijiji
hicho baada ya baadhi ya nyumba zao kuvunjwa na mawe makubwa
yanayoporomoka na maji kutoka milimani na mmomonyoko wa ardhi
uliozingirwa na mifereji ya maji, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha
kwa takriban siku 40 mfululizo kijijini hapo.
Akiongea
mara baada ya kukagua shughuli za urejeshaji wa hali na kabla ya
kukabidhi misaada kutoka Mfuko wa Maafa unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shuhghuli za Maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amesema katika menejimenti ya maafa hatua za
urejeshaji hali baada ya maafa zinazingatia urejeshaji ulio bora zaidi
kuliko wa awali hivyo kwa kuwa kijiji hicho kipo eneo hatarishi wananchi
hawanabudi kuishi eneo salama kwa afya zao na mali zao.
“Kwa
kuwa utabiri wa hali ya hewa unaonesha mvua za juu ya wastani
zitaendelea kunyesha hadi mwanzoni mwa mwakani, niitake Kamati ya maafa
ya wilaya kuhakikisha taratibu za kupima maeneo salama kwa wakazi wa
kijiji hiki zinakamilika kabla ya mwak huu kuisha ili wakazi wa kijiji
hiki waendelee kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa Taifa”
amesisitiza Kanali Matamwe.
Kanali
Matamwe ameeleza kuwa kwakuwa serikali imeamua kukihamisha kijiji hicho
ili wananchi hao waweze kuishi maeneo salama na wameanza kuwasaidia
wananchi hao kupitia Mfuko wa maafa unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu, amewataka wadau wengine kuendelea kuwasaidia wananchi hao ili
waweze kukamilisha ujenzi wa nyumba bora na salama katika eneo litakalo
ainishwa na serikali.
Ofisi
ya Waziri Mkuu , Kupitia Mfuko wa Maafa imeikabidhi Kamati ya Menejienti
ya Maafa ya Wilaya hiyo misaada kwa kaya zilizoathirika na maafa ya wa
mafuriko Wilayani humo ikiwa ni pamoja na magodoro100, bati 200,mikeka
200,blangeti 200,ndoo 200, sleeping bag 100 vikiwa na thamani ya
shilingi milioni kumi.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe,
Kissa Kasongwa aliishukuru ofisi ya Waziri Mkuu , Idara ya Uratibu wa maafa kwakuona umuhimu wa kuwasaidia waathirika wa mafuriko hayo Wilayani humona kwamba mahitaji hayo yemewafikia walengwa kwa wakati muafaka.
“Tumekuwa
tukifanya jitihada mbalimbali za kurejesha hali na sasa tayari Kamati
ya maafa ya wilaya tumeshaainisha eneo lenye ukubwa wa ekari 150 kwa
ajili ya kuanzisha kijiji kipya, lakini nimefuatilia nimeona bado
Halmashauri haijaenda kupima eneo hilo, nimemuelekeza mkurugenzi
jumatatu hii aende kwenye wnwo hilo nw upimaji uanze mara moja na zoezi
hili likamilike ” alisistiza Kasongwa
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Timotheo Mzava
alimshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera,
Bunge, kazi, ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama
ambaye ana dhamana ya kuratibu maafa nchini kwa kumsikiliza baada ya
kuwasilisha matatizo ya wananchi wake na hatimaye kuwatuma wasaisdizi
wake kwa ajili ya kushughulikia matatizo hayo ambapo maombi ya wananchi
hao yametekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.
Kwa
nyakati tofauti wakazi wa kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge, Aliamini
Mrutu na Asha Hizza wameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa misaada
waliyowapatia na kubainisha kuwa wako tayari kuhamia katika kijiji kipya
kitakacho anzishwa na serikali kwa kuwa wanapoishi sasa maisha yao yako
hatarini kw akuwa tayari kaya 63 nyumba zao zimeathirika huku kaya 38
hazina mahala pa kuishi.
Kwa
mujibu wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha
majukumu ya kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi
mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutafuta
rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika, pamoja
na Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za
dharura ndani ya Kijiji wilaya au mkoa. Pia kutoa taarifa za tahadhari
ndani ya eneo husika.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇