LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 30, 2019

JUMUIYA WA WAZAZI TANZANIA WAKUMBUSHIA OMBI LAO KWA MWENYEKITI WA CCM, RAIS DK. MAGUFULI LA KUONGEZEWA WABUNGE NA MADIWANI WA VITI MAALUM

CCM Blog, DAR ES SALAAM
Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wazazi Tanzania, imekumbushia ahadi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Dk. John Magufuli kuhusu utekelezaji wa ombi la kuongezewa wabunge na madiwani wa viti maalum sawa na idadi ilivyo kwenye Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM)

Mwaka 2017, Rais Magufuli alipokea ombi la jumuiya hiyo la kutaka idadi ya wabunge na madiwani wa viti maalum iwe inatolewa sawa na jumuiya nyingine za CCM za UVCCM na UWT zilizo ndani ya chama hicho.

Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongeza Rais Magufuli na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein kwa utekelezaji wa ilani ya CCM, Ijumaa Novemba 29, 2019 jijini Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ( pichani), amesema jumuiya zote zina nafasi sawa ndani ya CCM na wanataka wabunge hao wachaguliwe na Baraza kuu la chama hicho.

Amesema Jumuiya hiyo ya Wazazi Tanzania inaomba utekelezaji wa ahadi hiyo ufanyike mapema ili wanachama wake wajulishwe mapema.

"Jumuiya itafurahi utekelezaji ukifanyika mapema ili wanachama wajulishe na tufanye maandalizi mapema," amesema Dk. Mndolwa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages