Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Simiyu, alipowasili leo
kwa ziara ya kikazi inayohusu Jeshi la Magereza mkoani humo kuanza
kilimo cha pamba kwa kutumia ardhi na nguvukazi ya wafungwa
walionao.Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza wakati wa kikao cha kamati
ya Ulinzi na Usalama baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kushoto) alipowasili kwa lengo la
kujadili Jeshi la Magereza mkoani humo kuanza kilimo cha pamba kwa
kutumia ardhi na nguvukazi ya wafungwa walionao.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera (aliyevaa nguo ya
Kitenge), baada ya kukagua vyumba vya mahabusu na ofisi ya Polisi
wilayani hapo.Wengine ni Maafisa wa Jeshi la Polisi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(katikati),akitoka kuzungumza na mahabusu waliohifadhiwa katika Kituo
cha Polisi cha Wilaya ya Busega,mkoani Simiyu. Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi
…………………..
Na Mwandishi Wetu, Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amelitaka Jeshi la Magereza kutumia
jumla ya Ekali Elfu Tatu na Sabini na Moja zilizopo mkoani hapo kwa
kilimo cha pamba ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.John Magufuli
la kutaka jeshi hilo kubadilika na kuingia kwenye mfumo wa uzalishaji
ili liweze kuondokana na mfumo wa kutegemea bajeti kuu ya Serikali
kulisha wafungwa nchini.
Ameyasema
hayo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni mkoani hapo lengo ikiwa ukaguzi wa shughuli za
taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo na kuangalia fursa zinazopatikana
katika mikoa mbalimbali nchini ili kuweza kulibadilisha jeshi la
magereza
“Mheshimiwa
naibu waziri sisi kama mkoa tuko tayari kushikana na jeshi la magereza
kwani kuna ardhi ya kutosha na naomba nikuhakikishie hawa wakilima pamba
japo ekali mia moja tu na zikauzwa wataweza kufanya mambo mengi ya
maendeleo ikiwemo kujenga nyumba za kuishi askari ambazo zitakua ni za
kiwango cha juu,” alisema Mtaka
Akizungumza
katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi
Hamad Masauni alisema Serikali imelipokea jambo hilo kwani ndio lengo
hasa la serikali kuona jeshi la magereza linajitegemea katika uendeshaji
wake pasipo kutegemea bajeti kuu ya serikali
“Mheshimiwa
Rais alishatuagiza tulibadilishe jeshi hili la magereza na tayari
tushaanza na tumetenga magereza kumi ya kimkakati nchini ambayo
yameteuliwa kuleta mapinduzi katika jeshi, ziara hii ni kuona fursa
zilizopo katika mikoa mingine kupitia magereza,nakuahidi jambo hilo
tumelichukua kama wizara na muda si mrefu litapatiwa ufumbuzi,” alisema
Masauni
Naibu
Waziri Masauni pia alipata nafasi ya kutembelea Kituo cha Polisi cha
Wilaya ya Busega na kuzungumza na mahabusu waliopo kituoni hapo ambapo
akuridhishwa na hali ya uchafu katika chumba cha mahabusu kituoni hapo
na kuuagiza uongozi kufanya utaratibu wa kusafishwa kwani waliopo ndani
ni binadamu na wana haki zao ikiwepo kukaa sehemu safi ili kulinda afya
zao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇