Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwaapisha
Mahakimu Wakazi wa Mahakama za Mwanzo wapya leo Novemba Mosi, mwaka huu
katika ukumbi namba mbili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, iliyopo
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi na kulia ni Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe Beatrice Mutungi.
Mahakimu
Wakazi wa Mahakama za Mwanzo wapya wakila kiapo cha kuitumia kazi yao
leo Novemba Mosi, mwaka huu, katika ukumbi namba mbili wa Mahakama ya
Rufani Tanzania, iliyopo jijini Dar es Salaam.
Picha na Magreth Kinabo- Mahakama
……………..
Na Mary Gwera, Mahakama
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewaasa Mahakimu Wakazi
wa Mahakama za Mwanzo wapya kutokubali maelekezo ya aina yoyote kutoka
nje ya Mamlaka zao kuhusiana na mashauri yaliyopo mbele yao.
Akizungumza
na Mahakimu Wakazi hao ,wapya 23 mara baada ya kuwaapisha rasmi, mapema
Novemba 01, 2019 katika Ukumbi wa Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam,
Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa Mahakimu hao wana mamlaka ya kusikiliza na
kuamua mashauri bila kuingiliwa na yeyote.
“Jaji
au Hakimu lazima awe ni mtu wa kuheshimu mamlaka nyingine, vivyo hivyo
msikubali maelekezo ya aina yoyote kutoka nje ya Mahakama ama iwe Jaji
au mtu mwingine kuhusiana na kesi/mashauri yaliyopo mbele yenu,”
alieleza Mhe. Jaji Prof. Juma.
Mhe.
Jaji Mkuu aliongeza kwa kuwataka Mahakimu hao kutekeleza majukumu yao
bila upendeleo kwa kuwa ni jambo linalosababisha matabaka baina ya
watu/wananchi.
“Upendeleo
ni jambo la hatari sana, muwe wawazi, muwe wasikilizaji makini, lazima
muwasaidie wananchi ambao wengi hawajui sheria kwa kuwaelimisha,”
alisisitiza Mhe. Jaji Mkuu.
Hali
kadhalika, Mhe. Jaji Mkuu aliwapa angalizo Mahakimu hao juu ya uandishi
wa hukumu sahihi kwa kutumia lugha inayoeleweka ili wananchi/wateja
waweze kuelewa kwa urahisi.Masuala
mengine aliyowaeleza Mahakimu hao ni pamoja na kufanya tafiti, matumizi
ya TEHAMA na kuishi viapo vyao wanapotekeleza majukumu yao.
Jumla
ya Mahakimu Wakazi wapya 23 wameapishwa na wamepangiwa kufanya kazi
katika Mahakama za Mwanzo katika mikoa mbalimbali nchini
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇