RAIS
Dk. John Magufuli ameagiza majengo yote yaliyokuwa ya Ofisi za Wakala wa
Barabara Tanzania(TANROAD) eneo la Dumila mkoani Morogoro
yakabadilishwe na kuwa Kituo cha Afya Dumila.
Ametoa
maagizo hayo leo Novemba 20,mwaka 2019 wakati akizungumza na wananchi
wa Dumila akiwa safari kuelekea mkoani Dodoma.
Akiwa hapo wananchi hao
kupitia diwani wao walitoa maombi yao kadhaa kwa Rais ambayo kwao
yamekuwa changamoto ikiwemo ya kukosa kituo cha afya, uhaba wa maji safi
na salama na umeme.
Hivyo
wakati anajibu changamoto hizo, Rais amesema kuanzia leo hii, majengo
hayo ya ofisi za TANROAD yatakuwa Kituo cha afya Dumila na nyumba 11 za
ofisi hizo ziwe nyumba za watumishi wa kituo hicho.
"Hoja
zote ambazo zimetolewa na diwani wenu hapa ni za msingi na zitafanyiwa
kazi, hili la kituo cha afya, naagiza majengo ya ofisi ya Tanroad yawe
kituo cha Afya, kuhusu madaktari, dawa na vifaa tiba hilo nitatoa
maagizo kwa Wizara ya Afya.
"Kesho
Diwani mje mfungue kituo cha afya na andika jina lako kwa niaba yangu,
nimekuruhusu.Yale majengo yalijengwa kwa fedha za Serikali, kuna nyumba
11 nazo zote ziwe za kituo cha afya Dumila,"amesema Rais Magufuli.
Pia
Rais amesema changamoto nyingine ambazo zimeelezwa na wananchi hao
zitafanyiwa kazi huku akitumia nafasi hiyo kutoa ruhusa ya wananchi hao
kuchimba mchanga katika daraja la Mto Dumila ingawa ametaka kuwepo na
utaratibu mzuri ambao uchimbaji huo hautaharibu daraja hilo.
"Nawaruhus
mchimbe mchanga, lakini tukubaliane kwa utaratibu mzuri, tusiharibu
hili daraja.Ikitoke mkachimba mchanga na kuharibu daraja matipa yote
nitayakamata,"amesema Rais Magufuli.
Wakati
huo huo Rais Magufuli amewataka viongozi wa Mkoa wa Morogoro
wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo kutafuta ufumbuzi wa migogoro kati ya
wakulima na wafugaji ambao ametumia nafasi hiyo kueleza anayo matumaini
makubwa kuwa ufumbuzi utapatikana.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇