Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na washiriki wa
mafunzo ya wadadishi wa utafiti wa mwaka 2019 kwa niaba ya mkuu wa mkoa
wa Iringa ambaye hakuwepo kutokana na kuwa na majukumu mengine ya
kiserikali.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na washiriki wa
mafunzo ya wadadishi wa utafiti wa mwaka 2019 kwa niaba ya mkuu wa mkoa
wa Iringa ambaye hakuwepo kutokana na kuwa na majukumu mengine ya
kiserikali.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiagana na mtakimwi
mkuu wa serikali Dr Albina Chuwa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya
wadadishi wa utafiti wa mwaka 2019 kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa
ambaye hakuwepo kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kiserikali
Na Fredy Mgunda, Iringa
WATAFITI wote wanaofanya utafiti Tanzania wametakiwa kufanya utafiti
wakiwa wanaelimu ya utafiti kutoka chuo cha takwimu hapa nchini au nje
ya nchini kwa lengo la kuondoa takwimu zisizo sahihi ambazo zimekuwa
zikileta migogoro kwenye jamii.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wadadishi wa utafiti wa
mwaka 2019 kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa,mkuu wa wilaya ya Iringa
Richard Kasesela amesema kuwa watakwimu wote wanatakiwa kufanya tafiti
wakiwa na cheti kinachomsibitisha kuwa ni mtakwimu.
“Wanaojiita mtakwimu yeyeto yule lazima awe na cheti ambacho
kinamdhibitisha kuwa ni mtakwimu na amesaini maadili ya takwimu la sivyo
atakuchuliwe hatua za kisheria na pia hataruhusia kufanya kazi za
kitafiti katika eneo usiku” alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa watakwimu wakitoa takwimu ambazo sio sahihi
sinaleta tatizo kwenye usalama wa taifa kwa unakuwa umetikisa usalama wa
taifa.
“Huyu mama na watu wake ni muhimu sana kwa usalama wa nchini kwa kuwa
wanatoa takwimu zilifanyiwa kazi na zimethibitishwa na mamlaka husika”
alisema Kasesela
Aidha Kasesela amesema kuwa watafiti wengi wanatakiwa kurudi darasani
ili kuwasaidia kutoa takwimu zilizo sahihi na zisizoleta madhara kwa
usama wa taifa.
Awali akitoa maelezo kwa ufupi kwa mgeni rasmi,mtakimwi mkuu wa
serikali Dr Albina Chuwa amesema kuwa watatumia technolojia ya hali ya
juu kukusanya takwimu zilizo sahihi kwa muda mfupi.
“utafiti
huu kwa weledi wa juu wa kutumia teknolojia ya Kisasa ya kusanya
takwimu Nchi nzima kwa muda mfupi na kupunguza gharama na Utafiti huu
umgefanyika miaka kumi kumi iliyopita ungegharamiwa kwa Tshs. Bilioni 5
lakini kwa matumizi ya teknojia ya Tablets imepunguza gharama kwa
nusu,Utafiti huu utagharimu TShs. Bilioni 2 na Matokeo yatatolewa mwezi
Desemba 2019” alisema Chuwa
Hata hivyo Chuwa alisema dhahiri teknolojia kwa kiasi kikubwa
imepunguza gharama za kufanya Tafiti hapa Nchini na nitumie nafasi kutoa
wito kwa Watakwimu wote Nchini kuwa ni vyema tujikite zaidi katika
kuendeleza kujifunza zaidi teknolojia za kisasa za kuchakata taarifa za
Kitakwimu kwa kuwa kwa sasa Dunia kila siku mbinu mpya za kitakwimu
zinaendelea kufanyiwa majaribio na kutumika na Maofisi ya Takwimu
Duniani.
“Napenda kuwaomba Benki ya Dunia na IMF kuendelea kuzijengea uwezo
Ofisi za Takwimu za Afrika katika Matumizi ya teknojia mbali mbali za
kuchakata takwimu wakati tunapoelekea kutekeleza Malengo Endelevu ya
Maendeleo ya Dunia ya mwaka 2030” alisema Chuwa
Aidha Chuwa alisema kuwa hanashaka na matokeo ya Utafiti huu kwa kuwa
juhudi zinazoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya
Mpendwa wetu Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kupambana na uchumi
wa Viwanda asilimia za upatikanaji wa yakavuka malengo yaliyowekwa
katika Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Umeme hapa Nchini. Miradi ya
Kimkakati iliyoainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Maendeleo -2016/ 17
2020/21 umebainisha mikakati ya upatikanaji wa umeme wa kutosha hapa
Nchini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇