LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 19, 2019

BREAKING NEWZZZZZZ.. MEYA WA JIJI LA ARUSHA KALISTI LAZARO (CHADEMA) ATIMKIA CCM



Wakati kitimtim cha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kikiendelea nchini, Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro kwa tiketi ya Chadema, ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.

Akizungumza katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar esa Salaam, Kalisti Lazaro, ameeleza kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kupitia wakati mgumu akiwa katika wadhifa wake wa Meya wa Jiji la Arusha.

Amesema amepokea barua za maonyo mara kadhaa kutoka kwa uongozi wa Chadema, ambazo zilimtaka kutokutoa ushirikiano na Viongozi wa Serikali ambao anatakiwa kufanya nao kazi ngazi ya Mkoa na Wilaya na kutompongeza hadharani Rais Dk. John Joseph Magufuli kwa kazi nzuri ambayo ameifanya Nchini ikiwamo katika Mkoa wa Arusha.

Vitisho vya mara kwa mara ikiwamo dhidi ya uhai wake ndio vimepelekea kujivua nafasi zake zote katika Chadema na kujiunga na CCM, Chama ambacho kinashughulika na utatuzi wa kero za wananchi. Ndg. Lazaro pia amechukizwa na Chama chake kujitoa katika uchaguzi huku akiita kitendo hicho uvunjaji wa demokrasia ambacho ndani ya masaa mawili uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema iliwanyima mamilioni ya wapenda demokrasia haki ya kushiriki katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.

Ndg. Kalisti Lazaro amesema sasa yuko tayari kuchapa kazi ya wananchi akiwa ndani ya Chama ya Mapinduzi na kwamba yuko tayari kwa maelekezo ya kazi kutoka Uongozi wa CCM.

Ndg. Kalisti kwa kujiunga na CCM amejiuzuru nafasi ya Udiwani, Umeya wa Jiji la Arusha, Uenyekiti wa Mameya na Madiwani wote wa Chadema Nchini na Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.'

Ndugu Kalisti Lazaro atapokelewa rasmi na wanachama wa CCM Mkoa wa Arusha katika tarehe itakayopangwa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages