Kutokana na moto uliounguza vibanda vya wafanyabiashara Soko kuu Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi usiku wa kuamkia jana jumla ya shilingi milioni 100,550,000. ni thamani ya vitu vilivyoteketea kwa moto huo.
Akitoa tathmini hizo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Katavi Islael Kutika amesema uchunguzi Bado unaendelea kujua chanzo cha moto.
Kutokana na ujenzi holela wa vibanda katika Soko hilo jeshi la Zimamoto limetoa onyo kwa wafanyabiashara kufuata utaratibu maalum wa ujenzi wa vibanda kwa usalama wa bidhaa zao pindi tatizo linapotokea
Aidha Jeshi la Zimamoto limefanya juhudi kudhibiti moto huo na lita 102 za mafuta ya kula ndio zimeokolewa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇