Na Said Mwishehe,Michuzi TV.
WIZARA
ya Fedha na Mipango imtangaza kuwa sasa mfumo wa Serikali wa kufuatilia
utekelezaji wa taarifa za ukaguzi umezinduliwa rasmi huku ikisisitiza
kuwa wakaguzi wa ndani wa taasisi za umma wataanza kuutumia mfumo huo
kikamilifu na kuachana na utamaduni wa kuwalisha taarifa za ukaguzi kwa
mlipaji mkuu wa Serikali kwa kutumia nakala ngumu.
Akizungumza
wakati wa kuzinduliwa kwa mfumo huo leo Oktoba 31 jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango aliyekuwa mgeni rasmi
Amina Shaaban amesema kuwa mfumo huo utafanyiwa maboresho ili kuwaingiza
wadau wengine wa umma walio katika ofisi ya Msajili wa Hazina,
wasimamizi wa wakaguzi wa ndani na mamlaka za Serikali za Mitaa walio
katika sekretarieti za mikoa TAMISEMI na hata wakaguzi wakuu ili
kurahisisha utendaji kazi serikalini.
Pia
amesema Serikali itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo
kutenga fedha kupitia idara ya mkaguzi wa ndani mkuu wa Serikali kwa
ajili ya kuimarisha na kuboresha mfumo huo kuhakikisha kuwa watumiaji
wote wanapata mafunzo stahiki ambapo alitumia nafasi hiyo kueleza bado
kuna watumishi wengi hawana mafunzo kuhusu mfumo huo na hivyo
wataendelea kuelimishwa siku hadi siku.
"Nipende
kumshukuru Kaimu Mkurugenzi wa Ndani Mkuu wa Serikali kwa kunialika
katika kuzindua mfumo huu muhimu wa kufuatilia utekelezaji wa taarifa za
ukaguzi katika taasisi za umma(GARIITS).Natambua mkaguzi mkuu wa ndani
wa Serikali na wataalam wake kwa jinsi walivyoonesha umuhimu wa suala
hili na kuhakikisha kuwa wanasaidia mfumo huo wa kieletroniki wa
kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya wakaguzi wote wa ndani na nje
yanayotolewa kwenye taarifa zao za mara kwa mara. Pia natambua sheria ya
fedha ya mwaka 2010 iliweka jukumu la kumsaidia mlipaji mkuu wa
Serikali katika ya ukaguzi wa ndani katika masuala ya ukaguzi wa ndani
katika taasisi zote za umma,"amesema Shaaban.
Amefafanua
kuwa kuwamoja ya lengo kuu katika mpango mkakati wa Wizara ya Fedha na
Mipango wa mwaka 2017-2022 ni kuimarisha usimamizi wa masuala ya fedha
na uwajibikaji , hiyo inajumuisha kuimarisha mifumo ya kufuatilia
utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa ndani na wakaguzi wa nje wa taasisi
zote za umma.
Aidha
amesema Serikali imeweka utaratibu wa kuhakikisha kunakuwa na ufanisi
katika matumizi ya rasilimali za umma kupitia kufanya tathimini ya
utendaji."Kwa mantiki hii wakaguzi wa ndani katika taasisi zote za umma
wanatakiwa kutekeleza wajibu wa kuthamini na kutoa taarifa za
utekelezaji wa mapendekezo yaliyo katika taarifa za ukaguzi zilizotolewa
na wao hata zile zilizotolewa na wakaguzi wa nje na maelekezo
yanayotolewa na waangalizi wengine kama mamlaka za usimamizi na kamati
za Bunge,"amesema.
Pia
amesema ikumbwe kwamba Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa kuishia mwaka
2025 unasisitiza kuhusu utawala bora ni msingi muhimu na uwekaji wa
utamaduni wa uwajibikaji.Utawala bora ni msingi muhimu katika kusuma
mbele ajenda ya maendeleo ya nchi yetu.
Hata
hivyo amesema ili kuwezesha utekelezaji kikamilifu wa mapendekezo
yaliyotolewa katika taarifa za ukaguzi katika mnyororo wa uwajibikaji na
usimamizi bora wa masuala ya fedha ni wazi kuwa Serikali ilihitaji
mfumo madhubuti wa kukusanya taarifa sahihi za mapendekezo ya wakaguzi
yaliyotekelezwa na mapendekezo ambayo hayajatekelezwa kwa ajili ya
kufanya maamuzi sahihi.
"Mfumo
huu ambao nimeuzindua utakapatikana kwa njia ya mtandao mahali popote
alipo mkaguzi wa ndani wa taasisi za umma , utakuwa rafiki katika
kuutumia , utaweza kuboreshwa bila kutumia gharama kubwa na kuwaongeza
watumiaji wengine watakaoonekana ni muhimu na hauna gharama za mara kwa
mara za leseni,"amesema Shaaban.
Ameongeza
anazo taarifa kuwa pamoja na kuwa na Serikali inao wakaguzi wa ndani
zaidi ya 1,200 ni wakaguzi wakuu wachache tu wasiozidi 200 waliopatiwa
mafunzo ya matumizi ya mfumo huo na ambao kwa sababu wanautumia
kuwalisha taarifa zao kwa mlipaji mkuu wa Serikali.Pia amesema
amefuatilia mfumo huo bado unachangamoto chache zilizojitokeza baada ya
kuutumia kwa majaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Ametaja
baadhi ya changamoto hizo ni kutotambua wadau muhimu kama maofisa
masuuli, wasimamizi wa mashirika ya umma walioko katika ofisi ya Msajili
wa Hazina, wasimamizi wa wakaguzi wa ndani.Hivyo ni matarajio yake
baada ya uzinduzi huo changamoto hizo zitapata ufumbuzi wake kwa mfumo
kufanyiwa marekebisho ili kuwaungiza wadau wengi zaidi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ,Bi. Amina Shaaban
akizungumza mbele ya Wageni waalikwa (hawapo pichani), leo jijini Dar
wakati wa kuzindua rasmi mfumo wa Serikali wa kufuatilia utekelezaji wa
Taarifa za ukaguzi (Goverment Audit Report Implementation Information
Tracking Systtem-GARIITS). Wageni waalikwa hao pia Washirika wa
Maendeleo kupitia mpango wa kuboresha usimamizi wa Fedha za Umma
(Public Financial Reform Programme-PFMRP),waliotoa fedha za kutekeleza
wazo la Serikali kupitia kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali la kuwa
na mfumo huo.
Mkaguzi
Mkuu wa Ndani wa Serikali,Mhandisi Amin Mcharo akieleza namna ya
kutumia mfumo wa Serikali wa kufuatilia utekelezaji wa Taarifa za
ukaguzi (Goverment Audit Report Implementation Information Tracking
Systtem-GARIITS) mbele Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango ,Bi Amina Shaaban na Wageni waalikwa mbalimbali ambao ni
Washirika wa Maendeleo kupitia mpango huo wa kuboresha usimamizi wa
Fedha za Umma (Public Financial Reform Programme-PFMRP),waliotoa fedha
za kutekeleza wazo la Serikali kupitia kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa
Serikali la kuwa na mfumo huo.
Sehemu
ya Washirika wa Maendeleo kupitia mpango wa kuboresha usimamizi wa
Fedha za Umma (Public Financial Reform Programme-PFMRP),wakifuatilia
aliyokuwa akizungumza mgeni rasmi kuhusiana na mpango huo muhimu kwa
Serikali.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ,Bi. Amina Shaaban (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Washirika
wa Maendeleo kupitia mpango huo wa kuboresha usimamizi wa Fedha za Umma
(Public Financial Reform Programme-PFMRP),waliotoa fedha za kutekeleza
wazo la Serikali kupitia kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali la kuwa
na mfumo huo.Picha na Michuzi JR (MMG).






No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇