Serikali
ya Tanzania imesema inatambua umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya
mawasiliano kama mkakati mmojawapo wa kuhakikisha azma ya kuwa nchi ya
uchumi wa kati kupitia viwanda inafikiwa.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce
Ndalichako alipomwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa katika
ufunguzi wa Kongamano la Nne la Huduma ya Mtandao Jamii linalofanyika
katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo amesema sekta ya mawasiliano
ni moja ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi
nchini.
"Kwa
kipindi cha Julai hadi Desemba 2017 sekta ya mawasiliano ilikua kwa
asilimia 13.1 na ilikuwa sehemu ya pili katika kuchangia ukuaji wa
uchumi nchini," amesema Profesa Ndalichako.
Profesa
Ndalichako amesema katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika
mpaka vijijini, mwaka 2014 serikali iliingia mkataba na kampuni kutoka
Vietnam wa kuhakikisha huduma hiyo inafika katika vijiji 4,000 ambapo
kufikia Januari 2019, vijiji vyote vilikuwa vimefikiwa na huduma hiyo.
Waziri
huyo ameendelea kuelezea kuwa serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa
Wote (UCSAF) imefanya kazi kubwa katika kuhakikisha inafikisha
mawasiliano vijijini ambapo mpaka sasa imeweza kupeleka huduma ya
mawasiliano katika Kata 562 zenye vijiji 2,132.
Aidha,
Profesa Ndalichako amesema kwa upande wa elimu, mfuko huo umewezesha
kufika kwa huduma za mawasiliano katika baadhi ya shule na taasisi za
kielimu pamoja na kutoa mafunzo ya huduma za mawasiliano kwa walimu
wapato 1,229.
Akizungumza
katika Kongamano hilo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
Profesa Faustine Bee amesema kongamano hilo linatoa nafasi kwa washiriki
kujifunza namna ya kuendelea kuboresha huduma ya mawasiliano kwa jamii
hasa jamii ambayo haijafikiwa na huduma hiyo.
"Lengo
kubwa ni kuhakikisha ifikapo 2025 taasisi zote za serikali ziwe
zimefikiwa na huduma ya mawasiliano ikiwemo vyuo vyote, shule zote za
msi ngi na sekondari pamoja na ofisi zote za serikali," amesema Profesa
Bee.
Kongamano
hilo la wiki moja linahusisha nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa
Internet Societ Association for Progressive Community na ufanyika mara
moja kwa mwaka, ambapo kwa mwaka huu limefanyika nchini Tanzania likiwa
na washiriki kutoka Kenya, Uganda, Liberia, Cameroon, Ghana, Spain na
mwenyeji Tanzania.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako leo Oktoba
30, 2019 amefungua Kongamano la Nne la Huduma ya Mtandao Jamii
lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa niaba ya Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akijadiliana
jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Faustine
Karrani Bee wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Huduma ya Mtandao Jamii
lilofanyika Chuoni hapo.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika
picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la huduma ya Mtandao Jamii



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇