Na Happiness Shayo, Magu
Watumishi
wa Umma nchini wametakiwa kutumia vizuri rasilimali zilizopo katika
kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu
na Miongozo ya kiutumishi iliyopo.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao
kazi chake na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu kilichofanyika
katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Magu mkoani Mwanza.
“Tujenge
uzalendo kwa kutumia vizuri rasilimali wezeshi katika utendaji kazi
wetu, tupende na kuthamini ili kuharakisha maendeleo ya taifa” Dkt.
Mwanjelwa amesisitiza.
Aidha,
Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi hao kuwa wavumilivu katika utendaji
kazi kwani Serikali inatambua changamoto zinazowakabili na inaendelea
kuzifanyia kazi.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Dkt. Philemon Sengati amemuahidi Mhe. Dkt.
Mary Mwanjelwa kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa kwa maslahi ya Taifa.
“Nimefarijika
mno na hii ziara na nimeyapokea maelekezo kwa moyo mkunjufu kabisa, na
nikuhakikishie kwamba tutaendelea kufanya kazi kwa ubunifu” Dkt. Sengati
amefafanua.
Ziara
ya kikazi ya Mhe. Mwanjelwa mkoani Mwanza ni utekelezaji wa majukumu ya
ofisi yake ya kuhimizi uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa
Halmashauri ya Wilaya ya Magu (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi
kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu Mkoani Mwanza. Kulia ni
Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Balozi Mstaafu
Mhe. John Haule, Mhe. Khadija Mbarak na Mhe. Alhaj Yahya Mbila.
Baadhi
ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza
wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani)
alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Shule
ya Sekondari Magu Mkoani Mwanza.
Kamishna
wa Tume ya Utumishi wa Umma, Balozi Mstaafu Mhe.John Haule,
akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma, wakati wa
kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa na Watumishi wa Umma
wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza kilichofanyika katika
Shule ya Sekondari Magu.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya
ya Magu, Mhe. Dkt. Philemon Sengati wakati wa kikao kazi kati yake na
Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza
kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na menejimenti ya Halmashauri
ya Wilaya ya Magu kabla ya kikao kazi kati yake na Watumishi wa Umma wa
Halmashauri ya Wilaya ya Magu katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Magu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇