Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
amewataka Wakurugenzi wa halmashauri nchini kuelewa kuwa pamoja na
watumishi wa sekta ya ardhi kuhamishiwa Wizara ya Ardhi lakini bado wana
jukumu la kusimamia utendaji wa sekta hiyo.
Dkt
Mabula alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara katika halmashauri ya
jiji la Mwanza pamoja na Manispaa ya Ilemela akiwa katika ziara ya
kukagua utendaji wa sekta ya ardhi katika Kanda ya Ziwa inayojumuisha
mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara na Geita.
Alisema,
tangu watumishi wa sekta ya ardhi walivyohamishiwa Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakurugenzi wengi wa halmashauri wameona
kama wamejivua kusimamia utendaji wa watumishi wa sekta hiyo jambo
alilolieleza kuwa siyo sahihi kwa kuwa mamlaka ya upangaji Majiji, Miji
na Manispaa unabaki kwa halmashauri.
‘’kazi
pekee inayosimamiwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
kwa watumishi wa sekta ya ardhi ni katika masuala ya nidhamu na ajira
ambapo katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi anawajibika’’ alisema Dkt Mabula.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema katika kuboresha
sekta ya ardhi nchini huduma za sekta hiyo sasa zimesogezwa katika mikoa
badala ya kutegemea ofisi za Kanda alizozieleza kuwa ziko mbali kwa
baadhi ya mikoa jambo linalowafanya wananchi kushindwa kupata huduma kwa
urahisi.
Katika
kufanikisha hilo Dkt Mabula aliwataka Wakuu wa mikoa kuharakisha
uanzishwaji ofisi za mikoa kwa kutenga ofisi ili wananchi waweze kupata
huduma za ardhi bila usumbufu ambapo alitolea mfano wa mikoa ya Tanga,
Ruvuma, Mtwara na Simiyu kuwa tayari ishatenga ofisi kwa ajili ya mikoa
yake.
Kwa
upande wake Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo
alisema mkakati wa ofisi yake kwa mwaka huu ni kuhakikisha uanzishaji
ofisi za mikoa usaidie kupunguza changamoto za sekta ya ardhi katika
mikoa mbalimbali.
Akiwa
katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Dkt Mabula lielezwa
na Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi katika halmashauri hiyo
Shukurani Kyando kuwa, halmashauri hiyo imekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji hati, urasimishaji na upimaji maeneo mbalimbali ingawa imekuwa na changamoto kubwa ya utapeli unaofanywa na madali kwa kuuza kiwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja.
Hata
hivyo, alisema katika kukabiliana na utapeli huo tayari wamewakama
matapeli saba na baadhi yao tayari wamefikishwa katika vyombo vya sheria
huku mmoja akikabidhiwa kwa Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa
(Takukuru) na kuwataka wananchi wanaotaka kununua viwanja kuhakikisha
wanajiridhisha katika ofisi za ardhi ama ofisi za ardhi za kanda ili
kuepuka kutapelewa.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha Kayenze- Baze
jijini Mwanza kutoka
kwa Meneja wa Masuala ya fedha wa Kampuni ya Songoro inayojenga kivuko
hicho wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho jijini Mwanza
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akiangalia moja ya Majalada katika ofisi za Ardhi Jiji la Mawanza jana
akiwa katika ziara yake ya kuangalia utendaji kazi sekta ya ardhi katika
mikoa ya Kanda ya Ziwa. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana
Dkt Phillis Nyimbi.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa
ndani ya kivuko kipya cha Kayenze- Baze kinachotarajiwa kuanza
majaribio mwezi Novemba 2019 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa
kivuko hicho jijini Mwanza
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa
katika kivuko kipya cha Kayenze- Baze jijini Mwanza ambacho
kinatarajiwa kuanza majaribio Novemba 2019 wakati akikagua maendeleo ya
ujenzi wa kivuko hicho jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇