Na Bashir Nkoromo
Licha ya kwamba Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli tangu aingie madarakani amefanya mambo mengi makubwa ya kupigiwa mfano kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania, lakini bado wapo baadhi ya Watu wachache ambao wanadiriki kubeza juhudi hizo.
Wakati wapo baadhi ya wanaobeza jitihada hizo, lakini pia wapo tena wengi ndani na nje ya Tanzania ambao wanamsifu hadi 'kumvulia kofia' Rais Dk. Magufuli kwa uongozi madhubuti ulio na ufuatiliaji makini wa utendaji katika sekta mbalimbali za kujenga na kukuza uchumi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya usafiri na ufirishaji sambamba na uthibiti wa matumizi ya rasilimali za nchi na nidhamu kwa watumishi wa umma.
Kijana Dk. Prosper Kiramuu Mbowe (Pichani) ni miongoni mwa mamilioni ya vijana Watanzania ambao wanamuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kwa uongozi bora.
Dk. Prosper ni msomi wa kiwango cha juu ambaye mwaka jana (2018), alihitimu Shahada ya uzamivu (PhD) kuhusu udhibiti wa masuala ya utakatishaji fedha kwenye Benki kwa nchi za Kanda ya Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya na Uganda, amesema kuwa hatua anazochukua Rais Dk. Magufuli kudhibiti utakatishaji fedha na rushwa ni sahihi.
"Unaweza kuona kuwa licha ya kwamba sheria za kudhibiti utakatishaji fedha na rushwa zilikuwepo tangu siku nyingi lakini kwa kuwa zilikuwa hazisimamiwi vizuri wale wenye uwezo mkubwa kifedha, vyeo vya juu vya kisiasa, undugu au urafiki na baadhi ya viongozi wenye mamlaka ya juu, walikuwa wakijifanyia vitendo vya utakatishaji fedha na hivyo kujitajirisha kwa njia hiyo haramu", anasema Dk. Prosper.
Anasema, hali hiyo iliifanya Tanzania kuwa nchi iliyoongoza kwa vitendo vya rushwa na utakatishaji fedha katika Kanda ya Afrika Mashariki.
"Sasa kama Rais Dk. Magufuli amefanikisha kudhibiti rushwa bila shaka ukifanyika utafiti itaonekana wazi kuwa kiwango cha vitendo vya utakatishaji fedha kimeshuka sana katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa sababu rushwa ndiyo ilikuwa miongoni mwa vichocheo vikubwa vilivyokuwa vikiruhusu kufanyika utakatishaji fedha", amesema Dk. Prosper.
Amesema, pamoja na Rais Dk. Magufuli kudhibiti rushwa, hatua ya kuondoa alichokiita utitiri wa maduka ya kubadilishia fedha pia imesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti vitendo vya utakatishaji akisema kwamba baadhi ya maduka hayo ya kubadili fedha yalikuwa yakitumika sana kutakatishia fedha za kigeni.
"Kutokana na hatua alizochukua Rais Dk. Magufuli, hivi sasa siyo rahisi mtu kwenda benki akajichukulia mamilioni ya fedha bila kuulizwa fedha hizo alikozipata, tena siki hizi ukienda Benki kuchukua hata sh. milioni kumi kwa ajaili ya kununua gari lazima uulizwe ulikozipata. hii ni tofauti na zamani mtu alikuwa anajichukulia kiasi chochote haulizwi ili mradi anajulikana kuwa ni mwanasiasa au ametoa rushwa", amesema Dk. Prosper.
Anasema, kutokana na udhibiti huu katika masuala la fedha, ndiyo sababu sasa baadhi ya watu wanalalamika kuwa 'vyuma vimekaza' kwa sababu wale wote waliokuwa na biashara haramu biashara zao zimekufa au zimedoda.
"Ni kweli hali ya upatikanaji fedha hivi sasa ni ngumu, lakini ni ngumu zaidi kwa wale waliokuwa awakijipatia fedha kupitia shughuli au biashara haramu, lakini kwa awaliokuwa walkifanya shughuli au biashara halali fedha wanapata na hali zao za kifedha siyo ngumu", alisema Dk. Prosper.
"Kwa kweli kama ningepata nafasi ya kumshauri Rais Dk. Magufuli mimi nisingemshauri bali nimngemshawishi tu aendelee kufanya anavyofanya sasa kwa sababu ndiyo njia sahihi na pekee itakayoiwezesha Tanzania kutimiza lengo lake la kuwa nchi ya uchumi wa kati kwa njia ya kuwa na viwanda", Anasema Dk. Prosper.
Katika masuala ya siasa, Dk. Prosper anasema, hakuwahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, isipokuwa alikuwa amezama zaidi katika masuala ya masomo, hadi Februari 11, 2016 alipoamua kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Kweli mimi sikuwaga na 'interest' sana ya kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, lakini baada ya kuvutiwa na utendaji wa CCM ya sasa chini ya Mwenyekiti wake, Rais Dk. John Magufuli, mwaka juzi niliamua kujiunga na CCM kwa kukata kadi yenye namba 769785 pale tawi la CCM la Mbezi Kati.
Anasema, chini ya Dk. Magufuli CCM imeonyesha kuwa kwa dhati inairejea misingi yake iliyowekwa enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, akisema, siyo siri kwamba misingi ile bora kwa maendeleo ya Tanzania ilikuwa kwa kiasi fulani imekengeukwa.
KUMFAHAMU ZAIDI DK. PROSPER KIRAMUU MBOWE~BOFYA HAPA
Your Ad Spot
Oct 15, 2019
Home
featured
makala
MTAALAM WA UDHIBITI UTAKATISHAJI FEDHA KIJANA DK. PROSPER MBOWE AMFAGILIA RAIS DK. MAGUFULI
MTAALAM WA UDHIBITI UTAKATISHAJI FEDHA KIJANA DK. PROSPER MBOWE AMFAGILIA RAIS DK. MAGUFULI
Tags
featured#
makala#
Share This
About Bashir Nkoromo
makala
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇