Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan tarehe 27 mwezi huu anatarajiwa kufungua semina ya wajumbe wa chama cha wabunge wanawake wa Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika itakayofanyika katika mkoa wa Arusha uliopo kaskazini mwa Tanzania.
Akizungumza leo, Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa, semina hiyyo itawakutanisha washiriki 50 kutoka nchi 18 za Jumuiya ya Madola.
Nchi hizo nii Afrika Kusini, Botswana, Cameroon, Eswatini, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius na Msumbiji, Nyingine ni Namibia, Rwanda, Sierra Leone, Ushelisheli, Tanzania, Uganda na Zambia.
Kauli mbiu katika semina hiyo ni kkuboresha ushiriki wa wanawake katika michakato ya uchaguzi.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa, miongoni mwa malengo ya semina hiyo ni kuboresha ushiriki wa wanawake katika michakato ya uchaguzi ili kuongeza idadi ya wanawake katika vyombo na taasisi zenye maamuzi.

Aidha Spika Ndugai amesema kuwa, zipo changamoto nyingi zinazowakwamisha wanawake kushiriki michakato yya uchaguzi kkama wapiga kura na wagombea.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, semina hiyo itajadili changamoto zote pamoja na namna ya kuzipatia ufumbuzi.
Kwa mujibu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwa, mabalozi wan chi 17 za Afrika, mawaziri na viongozii mbalimbali wanawake, viongozi wa dini, baadhi ya watendaji wa serikali za mikoa, wilayay na mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kushiriki katika semina hiyo.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇