Polisi ya Burundi imetangaza kuwa, imeua wapiganaji kumi na nne na kuwakamata wengine wengi katika mapigano yaliyotokea wilayani Musigati katika mkoa wa Bubanza Magharibi mwa Burundi, kilomita zaidi ya 15 katika mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Vyombo vya usalama nchini Burundi vimetangaza kuwa, bundukki zisizopungua 11 na zana zingine za kijeshi zimekamatwa katika sokomoko hilo.
Moise Nkurunziza, naibu msemaji wa jeshi la polisi nchini Burundi amesema kuwa, wabeba silaha hao wanasadikiwa kuwa wametokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mapigano kati ya vikosi vya usalama na ulinzi vyya Burundi na kundi hilo la wapiganaji yalianza mapema asubuhi ya jana Jumanne katika mkoa wa Bubanza, lakini taarifa ya mapigano hayo haikuweza kutolewa papo hapo, kulingana na kile kilichoelezwa na jeshi kwamba, lilikuwa likisubiri kulitokomeza kundi hilo.

Baadhi ya duru zinasema kuwa, wapiganaji wengi walionekana katika Wilaya za Mpanda, Gihanga na eneo la Mitakataka, mkoani Bubanza nchini Burundi tangu mwishomi mwa wiki iliyopita wakijaribu kuingia katika msitu wa Kibira baada ya kuvuka Mto Rusizi unaotenganisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi.
Kundi la waasi la Red-Tabara limekiri kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa wapiganaji wake ndio waliokabiliana vikali na vikosi vya usalama na ulinzi vya Burundi katika mapigano yaliyotokea jana na kwamba wanaendelea kuingia nchini Burundi kwa lengo la kurejesha utawala wa sheria.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇