LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 16, 2019

MBUNGE MWAKANG'ATA AWAPATIA WANAWAKE MISAADA YA MABATI, SARUJI, FEDHA NA TAULO MKOANI RUKWA

 Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang'ata (kulia), akikabidhi kwa Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Laela, Sumbawanga Vijijini hivi karibuni. Omelina Mgawe, mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Kikundi cha akina mama wauza mboga  na nyanya wa kata hiyo. Pia alitoa msaada wa mabati ya kuezekea soko hilo, ili waondokane na adha ya kuuzia bidhaa zao juani.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa (CCM), Bupe Mwakang'ata (kulia), akikabidhi kwa Diwani wa Kata ya Laela, Sangu, msaada wa mabati 24 kwa ajili ya kuezekea jengo la Soko la Kikundi cha akina mama wauza mboga wa Kata hiyo, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, katika hafla iliyofanyika hivi karibuni.
  Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang'ata,  akizungumza katika mkutano na wanafunzi wa  Shule ya Sekondari Uchile ya Sumbawanga Vijijini . Katika mkutano huo ambao mada kuu ni ilikuwa kupiga vita mimba za utotoni, alikabidhi pia msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule hiyo.
 Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang'ata  akimkabidhi Mwenyekiti wa  Kata ya Mnokola, Teofrida Mbaule msaada wa sh. 500,000, za kuwawezesha wanawake kibiashara wa kata hiyo. Kata zingine nne zilizopata kiasi kama hicho ni; Kasamsama, Laela A, Miangalua na Laela B.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages