Mwanasheria
na Afisa Mlinda Mlaji wa Tume ya Ushindani (FCC) Exavery Ngelezya
(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu elimu ya utambuzi wa
bidhaa bora na bandia iliyotolewa kwa wananchi katika maonesho ya pili
ya viwanda vidogo (SIDO) Kitaifa 2019 yanayoendelea Uwanja wa Bombadia
Mkoani Singida. Kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma, Adefrida
Ilomo.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma wa FCC, Adefrida Ilomo akizungumza na waandishi wa habari.
Na Dotto Mwaibale, Singida
TUME
ya Ushindani (FCC) imetoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali katika
maonesho ya pili ya viwanda vidogo (SIDO) Kitaifa 2019 mkoani Singida
kuhusu bidhaa bandia.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana katika maonesho hayo Afisa Mawasiliano na
Mahusiano ya Umma wa tume hiyo Adefrida Ilomo alisema tume hiyo imetoa
elimu kwa wananchi kuhusiana na utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu
wa sheria.
"Tumekusudia
kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda letu inayohusu masuala ya
ushindani, utetezi wa mlaji na udhibiti wa bidhaa bandia" alisema Ilomo.
Ilomo
alisema tume hiyo imeanza kutoa elimu ya wajibu wa wazalishaji na
wajasiriamali katika kusajili nembo zao ili waweze kulindwa na sheria ya
alama za bidhaa dhidi ya wazalishaji wanaoiga bidhaa zao kwa nia ya
kudanganya au kutapeli.
Alitaja
wajibu mwingine wa wazalishaji au wajasiriamali ni kuhakikisha
wanaonesha taarifa zote muhimu katika vifungashio kwa mujibu wa sheria
au alama za bidhaa ya 1963 na sheria ya ushindani ya mwaka 2003 na kuwa
wajibu wa wafanyabiashara na watoa huduma ni kuwasilisha taarifa zao kwa
ajili ya mapitio ya mikataba yote ya mlaji.
Mwanasheria
na Afisa Mlinda Mlaji wa FCC Exavery Ngelezya alitoa wito kwa wananchi
kutambua bidhaa bora na kuzibaini zile za bandia ili kuepuka madhara
yatokanayo na bidhaa hizo bandia.
Kwa
upande wa wajasiriamali wametakiwa kuhakikisha kutomlisha mlaji bidhaa
zisizo na ubora hivyo ni vyema kupitia taratibu zote kabla ya kupeleka
bidhaa zao sokoni
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇