TAASISI ya Wajasiriamali ya Kipinet imekutana na wajasiriamali 400 kwa ajili kuboresha biashara ili ziweze kuleta tija ya kujikwamua na umasikini .
Akizungumza na wajasiriamali hao Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Charles Sabiniani amesema kuwa fursa za biashara no nyingi sana hivyo kunahitaji kujitoa katika kufanya biashara.
Amesema kuwa jamii ina mahitaji mengi ambayo kwa wajasiriamali in fursa katika kubuni vitu ambavyo vitasaidia jamii hiyo kuondokana na ukosefu wa bidhaa.
Sabiniani amesema kuwa Kipinet iko katika kushika bega wasariamali katika kutoa mafunzo ya biashara mbalimbali zikiwemo za ubunifu bidhaa mbalimbali katika kutafuta masoko.
Aidha amesema kuwa wanawake ndio walezi wa familia hivyo ni lazima mjitume katika kupiga vita umasikini ndani ya familia.
"Kipinet tutahakikisha biashara zinasimama na kuleta mafanikio kutoka wajasiriamali wadogo mpaka wakubwa na taifa kuweza kupata maendeleo kutokana na kodi" amesema Sabiniani.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kipinet Charles Sabiniani akizungumza na wajasiriamali kwa ajili ya maonesho ya Biashara yatakayofanyika Novemba 7 hadi 10 katika Hoteli ya Travertine Magomeni Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika mkutano kuhusiana maandalizi ya maonesho ya biashara.
Wajasirimali wa Taasisi ya Kipinet wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Charles sabiniani kuhusiana na elimu ya vifungashio kuelekea maonyesho ya wajasiriamali yatayofanyika Novemba 7 hadi 10 katika vya Hotel ya Travertine Magomeni jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇