Mkuu wa mkoani Njombe Christopher Olesendeka
NJOMBE
Mkuu
wa mkoa Njombe Christopher Olesendeka ametoa siku mbili kwa wadaiwa
sugu waliosababisha kufilisika kwa benki ya wananchi Njombe NJOCOBA
kujisalimisha wenyewe octoba 22 saa nne asubuhi katika ukumbi wa
halmashauri ya wilaya ya Njombe ili kuweka maridhiano ya lini
watazirejesha fedha hizo huku pia akitoa onyo kwa yeyote atakae puuza
wito huo kukumba na nguvu ya vyombo vya dola.
Akizungumza
katika kikao cha ushauri wa barabara RCC mkoa wa Njombe Christopher
Olesendeka amesema Benki ya Njocoba ambayo ilikuwa tegemeo kubwa kwa
wakazi mkoani humo haiwezi kufia mikononi mwake na kuwakosesha huduma
wananchi hivyo ameanza msako wa watu waliohusika kuifilisi ili waweze
kuweka makubaliano ya lini watarejesha fedha walikopeshana kienyeji na
kwa kujuana bila kuzingatia taratibu.
Wakati
akitangaza siku ya jumanne kukutana na wadaiwa sugu wa benki ya
NJOCOBA, Olesendeka pia ametangaza octoba 24 kukutana na viongozi wa
vyama vyote vya ushirika ambavyo vimekufa kutokana na utaratibu mbovu
wa ukopeshaji fedha pamoja na matumizi mabovu ya fedha na kwamba
kiongozi ambaye hataona umuhimu wa kufanya hivyo jeshi la polisi
limkamate na kumtia mbaroni kwa masaa kadhaa.
Kwa
upande wao wakazi wa mji wa Njombe akiwemo Odilo Mathias wanasema
uamuzi uliochukuliwa na serikali ni uamuzi mzuri na wenye tija kwa
wananchi kwa kuwa ilikuwa ikitoa huduma za pembejeo za kilimo, elimu ya
fedha pamoja na kuweka na kukopa.
Aidha wamesema kufungwa kwake kumeathiri mzunguko kwa fedha kwa kuwa imefungwa na fedha nyingi za wateja wake.
Hatua
hiyo inapokelewaje na wakazi wa mji wa Njombe , hapa ni baadhi yao
akiwemo Odilo Mathias na Rozana ngimbuzi wanaeleza hisia zao.
Benki ya wananchi Njombe ilifungwa na BOT mwaka 2017 baada ya kubainika kuwa imeshindwa kujiendesha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇