Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kufungua Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Nakonde Zambia
NA K-VIS BLOG, TUNDUMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Edgar Lungu, leo hii Oktoba 5, 2019 kwa pamoja wamezindua kituo cha forodha cha pamoja cha huduma (One Stop Border Post) kwenye mpaka wa Tunduma/Nakonde.
Katika hafla hiyo, Marais wote wameonyesha matumaini yao kuwa kituo hicho kitaimarisha shughuli za kibiashara hapo mpakani na kurahisisha utoaji wa huduma.
Akizunghjmza kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli aliwahimiza wananchi wa nchi hizi mbili kutumia miundombinu hiyo ili kufanya biashara kwa kiasi kikubwa.
“Tanzania na Zambia tuna historia toka wakati wa harakati za ukombozi kusini mwa Afrika chini ya waasisi wa Mataifa haya mawili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kenneth Kaunda, na badae tumeendelea kuwa washirika wa kiuchumi.” Alisema Rais Magufuli,
Kwa upande wake, Rais wa Zambia Mhe. Edgar Lungu alisema, kabla ya ujenzi wa kituo hicho iliwachukua madereva wa malori siku tatu hadfi nne ili kuvuka mpaka lakini sasa iyakuwa siku moja tu kwa dereva kuvuka mpaka.
Aidha alionyesha furaha yake kutokana na ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizo mbili na kutolea mfano wa Bomba la Mafuta la TAZAMA ambalo lilijengwa enzi za utawala wa waasisi wa mataifa ya Tanzania na Zambia na mpaka leo bomba hilo limekuwa likifanya kazi vizuri, pia reli ya TAZARA.
Kituo hicho kimejengwa kwa ufadhili wa Taaisi ya TRADE MARK EAST AFRICA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika eneo hilo la Tunduma mkoani Songwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.
Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu wakati wakisalimia wananchi mara baada ya kuwasili katika Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.(PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇