LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 2, 2019

Mbwana Samatta: KRC Genk kuminyana na Napoli usiku wa leo


Samatta
Haki miliki ya pichaTF-IMAGES
Image captionSamatta tayari ameshafunga goli moja kwenye michuano ya Champions League
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa leo akiwa na klabu yake ya KRC Genk anatarajiwa kushuka dimbani kwa mchezo wake wa pili wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (Champions League) dhidi ya Napoli.
Genk, itakuwa nyumbani Ubelgiji katika dimba la Luminus Arena ikiwakaribisha miamba kutoka Italia klabu ya Napoli.
Katika mchezo wake wa kwanza Genk iliangushiwa kichapo kizito cha goli 6-2 ugenini dhidi ya RB Salzburg, huku Samatta akifunga goli moja la kufutia machozi
Katika mchezo huo, Samatta aliweka rekodi binafsi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Champions League na kufunga goli.
Napoli wao walianza kwa kuwafunga mabingwa watetezi Liverpool goli 2-0.
Hivyo, Genk hii leo watakuwa tena na kibarua kizito cha kuwazuia Napoli.
Hata hivyo, japo Genk haijawahi kupata ushindi hata mechi moja ya Champions League katika mara zote tatu walizoshiri michuano hiyo, wamefungwa mechi moja tu nyumbani kati ya sita walizocheza na kutoka sare tano.
Napoli pia hawajapata ushindi wakiwa ugenini kwenye hatua ya makundi ya Champions League katika mechi sita zilizopita. Hivyo, japo si ya kutumainia, historia inaweza kuwabeba Genk na kupata walau sare.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages