MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi wa meza kuu
(kulia kwa Rais) Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Balozi
Seif Ali Iddi na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr. Abdalla
Juma Mabodi wakiwa katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM
Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAJUMBE
wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, wakipitia
makabrasha ya Kikao cha Kamati Maalum ya CCM,wakiwa katika ukumbi wa
mkutano wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, kabla ya kuaza kwa Kikao
hicho.(Picha na Ikulu)MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi.MheDk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na kufungua Kikao cha
Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika katika
ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.kulia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe.Samia
Suluhu Hassan na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar.Mhe.Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu).
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana
na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.Bi. Lela Burhani Ngozi, alipowasili
katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, kuhudhuria Kikao cha
Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika leo
20-10-2019 katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu)
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo Tarehe Octoba
20,2019 ameongoza Kikao Maalumu cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa Zanzibar.
Kikao
hicho cha siku moja kimeanza majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa
Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na Wajumbe wa
Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.
Kupitia
Kikao hicho Makamu Mwenyekiti Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kikao
hicho ni mwendelezo wa kujadili baadhi ya ajenda zilizotokana na kikao
kilichopita ambazo zilitakiwa kufanyiwa kazi kwa mujibu wa maelekezo ya
Kikao hicho.
Kikao
hicho ni maalumu kinachojadili masuala mbali mbali ya Chama kwa mujibu
wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977 Toleo jipya la 2017.
Viongozi
mbali mbali Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan
ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇