LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 24, 2019

MAITI 39 ZAPATIKANA NDANI YA LORI KUSINI MWA UINGEREZA, DEREVA AKAMTWA

Kamanda mkuu wa polisi katika mji wa Essex, Andrew Mariner amesema maafisa usalama walikamata lori hilo lililokuwa limebeba miili 39 katika eneo la viwanda la Waterglade mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wahudumu za ambulensi katika eneo la viwanda la Waterglade.
Amesema uchunguzi unaendelea ili kuweza kuwatambua wahanga hao.
Kulingana na ripoti ya awali ya uchunguzi, lori hilo lilitoka Bulgaria na liliingia Uingereza Jumamosi, Oktoba 19 likipitia Holyhead, bandari inayopatikana kwenye pwani ya magharibi mwa Uingereza.
Dereva, mwenye umri wa miaka 25, mwenye asili ya Ireland Kaskazini, amekamatwa na polisi ya Uingereza akihusishwa na mauaji hayo.
Moja ya malori yanayotumiwa na wahajiri katika safari hatarishi za kwenda Ulaya
Miongoni mwa maiti hizo ni mwili wa mtoto mwenye umri wa miaka 10, huku baadhi ya duru za habari zikisema kuwa ni kijana barobarobaro.  Wahamiaji wengi wamekuwa wakijaribu kuingia Ulaya katika miaka ya hivi karibuni kwa kujificha katika makasha ya malori au kwa usafiri hatarishi wa boti za plastiki.
Miezi kadhaa iliyopita, wahajiri saba wa Kiafrika walipoteza maisha baada ya kukosa hewa wakiwa ndani ya lori lenye jokofu kwa muda wa siku mbili katika pwani ya Libya,  wakisubiri kupelekwa kutafuta kazi na maisha mazuri barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages