Na Humphrey Shao,Jamhuri Digital.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto leo amefanya ziara katika
Machinjio ya Vingunguti kukagua namna jinsi ujenzi unavyondelea na
kuzungumza na wamachinga na Mama lishe namna Manispaa ilivyojipanga
kuboresha eneo la kufanyia biashra ndani ya siku saba.
akizungumza
na wafanyabiashara hao Mstahiki Meya, Omary Kumbilamoto amesema kuwa
manispaa imeamua kuboresha eneo la nje ya machinjio ambapo vijana na
mamalishe wanafanya biashara zao ambalo kwa sasa lipo katika mazingira
mabovu.
"Nimekaa
na Mkurugenzi wangu tukaona si vyema hapa panajengwa machinjio ya
kisasa halafu hatua chache tu wenye nchi yao mnafanya biashara katika
mazingira magumu, hivyo tunawaomba mtupishe kwa muda wa siku saba ili
turekebisha eneo hili kwa kujenga vizimba vya mama lishe na vya kuchomea
nyama pamoja na kuweka paa la juu ili tuweze kuwawekea mazingira bora
ya kufanya kazi" amesema Kumbilamoto.
Pia
kumbilamoto alipata fursa ya kutembelea eneo ambalo machinjio mapya
yanajengwa na kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi na kusema kwa uharaka
huo anaamini mafundi hao wa shirika la nyumba la Taifa watamaliza
ujenzi huo ndani ya muda uliopangwa kama Mh Rais Dk. John Pombe Magufuli
alivyoagiza.
Aidha
kumbilamoto alipata fursa ya kutembelea eneo ambalo wanataraji
kuwahamishia wauza nyama inayochinjwa katika machinio hayo ya kisasa
hili wasiwe mbali na eneo lao .
Amesema
machinjio mapya yamekuja na changamoto nyingi hivyo nasi tunakabiliana
nazo kama viongozi hivyo tupo katika mazungumzo na watu wa Wizara ya
Kilimo hili waweze kutupatia eneo lao lililopo jirani na machinjio hili
tuweze kujenga soko la kuuzia nyama kwa muda wakati marekebishi ya soko
lao yakiwa yanaendelea.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akivuka vidimwi vya maji kukagua eneo la wafanyabiashra ndogondogo nje ya machinjio ya Vingunguti
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na
wafanyabishara waliopo nje ya machinjio ya Vingunguti ambao wanataraji
kuboreshewa eneo lao la lufanyia kazi.
Mmoja
ya Mama Lishe wanaofanya biashara katika eneo hilo akimshukuru Mstahiki
meya kwa hatua ya waliyofikia kuwaboreshea eneo lao la Biashara.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua eneo la Wizara ya Kilimo ambalo wauza nayama wanatakiwa kuhamishiwa kwa muda
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza jambo na mkandarasi anayejenga Machinjio ya Vingunguti kutoka shirika la nyumba la Taifa
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akipasua mawe katika site ya ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇