Anaandika Abdullatif Yunus, Michuzi TV KAGERA.
Miongoni
mwa majengo saba ya Vituo vya Umahiri (Centers of Excellence)
yanayojengwa hapa Nchini, chini ya Wizara ya Madini likiwemo jengo
lililojengwa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, limekabidhiwa rasmi na
kupokelewa na Waziri mwenye Dhamana Mhe. Dotto Biteko mapema Oktoba 04,
2019.
Jengo
hilo lenye Orofa tatu, lenye thamani ya Sh. Bilioni 1.081 ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyetaka
kuona mabadiliko katika Sekta ya madini kwa kuweka mazingira wezeshi.
Akizungumza
kabla ya kukabidhiwa jengo hilo, Waziri wa Madini Dotto Biteko
amepongeza usimamizi wa Jengo hilo kwa ujumla, huku akikumbusha nia ya
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutaka kujengwa kwa Vituo hivyo Saba,
lengo likiwa kuifanya Sekta ya madini iwe sekta ya wadau na wachimbaji
wa uhakika, na kuondokana na ujanja ujanja uliokuwa ukifanywa awali,
kufuatia nia hiyo pamoja na mambo mengine tayari leseni 12000 zimefutwa
na zitagawiwa Kwa wachimbaji wadogo, huku miongoni mwa hizo leseni,
leseni 156 ni kutoka Mkoani Kagera.
Aidha
Waziri Biteko ameongeza kuwa mpaka sasa Masoko zaidi ya 28 yameanzishwa
na vituo vidogo zaidi ya 18 vya kununua madini vimefunguliwa, ambapo
utaratibu mwingine wa kupata cheti cha uasilia kwa ajili ya kuanza
kupeleka madini hayo nje yakiwemo ya TIN umekamilika na kufikia
mwishoni mwa Mwaka huu Wizara itaanza kusafirisha madini nje ya Nchi,
Hivyo kukamilika kwa jengo hilo ni fursa kwa wachimbaji na
wafanyabiashara kuongeza ufanisi katika shughuli zao, na kuwataka
kulitumia jengo hilo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Awali
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema nia ya
Mkoa ni kuongoza Mikoa yote katika ukusanyaji madini, kwa kutoa elimu
kwa wachimbaji wa madini wadogo na wakubwa bila kutumia nguvu kubwa,
ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi huku suala la kudhibiti
utoroshaji wa madini likizidi kuimarishwa, na wito ukizidi kutolewa kwa
wawekezaji wa biashara ya Madini kuendelea kwekeza katika Sekta hii ya
Madini Mkoani Kagera.
Jengo
hilo lenye Ofisi za Maafisa madini na wataalamu, Ukumbi wa mikutano,
eneo la mafunzo, Chumba maalumu la kuhifadhi madini (strong room) pamoja
na huduma nyinginezo tayari limekabidhiwa kwa Wizara ya Madini kutoka
kwa Wajenzi wa Jengo hilo Shirika la Suma JKT, na tayari Wizara
imekabidhi kwa Tume ya Madini Mkoa wa Kagera tayari kwa matumizi.
Pichani
Waziri wa Madini Dotto Biteko akikabidhi funguo kwa Tume ya Madini mara
baada ya kukabidhiwa toka Suma JKT ambao ndio wajenzi
Pichani
In meneja mradi kutoka shirika la Suma JKT Kapteni Fabian Buberwa
akiwasilisha taarifa yake mbele ya Viongozi kabla ya kukabidhi mradi wa
jengo la umahiri.
Pichani
Waziri wa Madini Dotto Biteko akipokea funguo toka kwa Meneja mradi
Kapteni Fabian Buberwa kama ishara ya kukabidhiwa Jengo la umahiri mara
baada ya Kumalika ujenzi wake.
Pichani Ni Msafara wa Waziri wa Madini Dotto Biteko ukiwasili kukabidhiwa jengo la Umahiri, baada ya kukamilika kwa ujenzi.
Pichani ni Mhe. Ditto Biteko Waziri wa Madini akitoa nasaha zake mapema kabla ya kukabidhiwa Jengo la umahiri.
Pichani
Bi Veronica Nangale Kaimu Meneja Mradi akiwasilisha taarifa ya Ujenzi
kwa Viongozi mapema kabla ya kukabidhiwa kwa Jengo la umahiri.
Pichani
ni Muonekano wa Jengo la Orofa Tatu lenye thamani ya Shilingi Bilioni
1.081 lilojengwa Mkoani Kagera, chini ya Wizara ya Madini likiwa tayari
kwa matumizi baada ya kukabidhiwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇