
Komboa masafa marefu la Iran la kupiga vyombo vya majini kutokea nchi kavu.
Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Amir Hatami amesema kuwa, vitisho vya hivi karibuni vya rais wa Marekani, Donald Trump vya kutaka kuishambulia kijeshi Iran ni upayukaji tu wa kujaribu kuficha kufeli siasa za Washington mbele ya taifa hili la Kiislamu.
Matamshi hayo ya waziri wa ulinzi wa Iran yametolewa kujibu madai ya siku ya Jumatatu ya rais wa Marekani aliyejigamba kwamba eti anaweza kuanzisha vita vipya ikibidi kufanya hivyo.
Trump alisema, hivi sasa anaendesha zoezi la kuwarejesha nyumbani wanajeshi wa Marekani lakini akaonya kuwa nchi hiyo inaweza kuanzisha mara moja vita vipya.

"Tunaweza kuingia vitani. Tumejiandaa vizuri kuliko wakati mwingine wowote. Kama Iran itafanya kitu, watapigwa kwa namna ambayo hawajawahi kupigwa mfano wake huko nyuma," alipayuka hivyo Trump katika kikao cha baraza lake la mawaziri.
Hata hivyo waziri wa ulinzi wa Iran ameionya Marekani kwamba majibu ya taifa la Iran yatakuwa makala mno iwapo Washington itafanya kosa la kulishambulia kijeshi taifa hili.
"Iwapo watafanya kosa hilo, watapata majibu yatakayowaaibisha zaidi kuliko wakati wowote huko nyuma," amesema kwa kujiamini Brigedia Hatami.
Amesisitiza kuwa, majeshi ya Iran yamesimama imara kulilinda taifa na mipaka yote ya nchi na viko tayari kutoa majibu makali kwa vitisho na uchokozi wowote ule.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇