Na Karama Kenyunko,Michuzi TV
MKURUGENZI wa Mashtaka nchini Tanzania, Biswalo Mganga, amewaonya mawakili wa kujitegemea wanaochukua fedha kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi wanaoomba msamaha na kukiri makosa yao kwa kudanganya kuwa wanazipeleka fedha hizo kwa DPP au Ofisi ya DPP kuacha tabia hiyo mara moja kwani wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria
DPP Mganga ameyasema hayo leo Oktoba 3,mwaka 2019 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambapo pia ametumia nafasi hiyo kueleza wakati wanaendelea na zoezi la watu walioloomba msamaha na kwenda mahakamani kukiri na kuamriwa aidha walipe fedha au amri nyingine yoyote ile kwa nafuu ambayo watakayokuwa wamekubaliana imebainika kuna baadhi ya watu wakiwemo mawakili ambao wamekuwa wakitumika kutaka kukwamisha mchakato huo.
"Tumepata taarifa kuna baadhi ya mawakili wamekuwa wanachukua fedha kwa washtakiwa wanasema wanazipeleka kwa DPP au katika ofisi ya DP, naomba niwakanye au niwaonye wasirudie, wanaofanya hivyo, wanatafuta ugomvi na tayari nimeishaanzisha uchunguzi wasije tukalaumiana", amesema.
Pia amewewataka mawakili kufanya shughuli zao za ki uwakili bila kuathiri heshima ya watu wengine au ofisi anayoiongoza. Amesema utaratibu wa mshtakiwa kukiri uko pale pale, utaratibu wa kulipa malipo atapewa mahakamani si kwa Wakili ama mtu yeyote atoke na kwenda gerezani au kuwafuata ndugu na kuwaambia wampatie fedha akidai kwa madai anazipeleke banki, utaratibu huo haupo, ni vizuri watu wakajiepusha.
Aidha ameongeza kwa kuliangalia hilo, Serikali imefungua akaunti maalumu BOT, ambako fedha zote zitakazokuwa zinalipwa kwenye zoezi hilo zitapelekwa, na wala si kwenye akaunti ya Mahakamaha au viongozi wa juu wa Mahakama pamoja na viongozi wengine serikalini na wote wamejulishwa.
"Hakuna fedha itakayolipwa kwenye akaunti ya Mahakama ya ofisi ya DPP wala TRA zaidi ya hiyo ya BOT, hivyo atakayelipa kwingine huko tusilaumiane. Niwaombe tena, si mawakili wa Serikali, si watumishi wa ofisi hii au mtu yeyote yule atakayefanya vitendo vya namna hii nikamvumilia, hatutamvumilia mla rushwa," amesema DPP.
Alipoulizwa kuhusu watu ambao siyo washtakiwa lakini wametangaza kwamba wanataka kurudisha fedha ambazo walipewa na washtakiwa kwake. Amesema, mtu kama anajua alifanya makosa huko na anaona hataki kuendelea kuwa na uchafu, kitu kinachomkereketa rohoni na amegundua unamzuaje asirudishe hizo fedha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇