Na Ramadhani Kissimba na Eva Valerian, Washington Dc
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) ameitaka Benki ya
Dunia kujikita zaidi katika kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania
ili kuweza kuwainua kiuchumi wakulima hasa wale wa kati na wadogo.
Dkt.Mpango
aliyasema hayo wakati wa kikao cha majadiliano na timu nzima ya Benki
ya Dunia ambayo inafanya kazi nchini Tanzania na wengine kutoka Makao
Makuu ya Benki hiyo nchini Marekani.
Mhe.Mpango
alisema katika mkutano huo walipitia kwa pamoja utekelezaji wa miradi
mbalimbali inayoendelea hivi sasa inayofadhiliwa na Benki ya Dunia,
lakini pia walipitia na kujadili miradi ambayo inaanza kufikiriwa kwa
ajili ya utekelezaji kwa mwaka utakaofuata.
‘’Moja
ya vitu vilivyonifurahisha mwaka jana kwenye mjadala niliwaaomba sana
kwamba hatuwezi kuendelea kuitaka Benki ya Dunia isaidie kwenye miradi
mingine tu ni lazima nguvu kubwa ielekezwe pia kwenye miradi ya kilimo
ambayo kwa sasa msaada wa Benki ya Dunia katika miradi hiyo ni kidogo
sana’’ alisema Dkt.Mpango.
Aidha
Dkt.Mpango alielezea dhamira ya Tanzania kushirikiana na Benki ya Dunia
ili kuanzisha programu itakayohakikisha kuwa tija inapatikana kwenye
sekta nzima ya kilimo na mifugo, lakini pia kuweza kuyafikia masoko kwa
mazao yanayozalishwa nchini, hasa yale yenye thamani kubwa duniani.
Dkt.
Mpango amefafanua kuwa Benki ya Dunia imeridhishwa na kasi ya mabdiliko
inayofanyika katika sekta ya kilimo kwa maana ya uzalishaji kuongezeka,
lakini vile vile wakulima wa kati wamezidi kuongezeka.
Aidha,
kuongezeka kwa maeneo ya kilimo imewafurahisha wataalamu wa Benki hiyo,
ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa aina ya mazao yanayolimwa hasa
yale yenye thamani kubwa ambayo yanalimwa kwa kasi kubwa sana kuliko
ilivyokuwa awali.
Pia
Dkt. Mpango alisisitiza kuwa, Benki ya Dunia imeshafanya utafiti wao wa
kutosha ambao umeonesha kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo
kwa maana ya uzalishaji kuongezeka.
Mhe.
Mpango aliishukuru Benki ya Dunia kwa kukubali tena kuleta timu ya
wataalamu nchini Tanzania ambayo itakaa na sekta nzima ya kilimo na
ufugaji ili kuona ni namna gani hasa Benki ya Dunia itasaidia kuinua
sekta hiyo, na kuwasaidia wakulima hasa katika matumizi ya nguvu kazi
kwa upande mmoja na kuwaongezea kipato kwa upande mwingine.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifuatilia
majadiliano katika Mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya
Afrika uliofanyika Jijini Washington DC. Kulia kwa Mhe.Mpango ni Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolf Ndunguru na
anayefuatia ni Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw.
Msafiri Mbibo.
Mtaalam wa Masuala ya Kilimo kutoka Benki ya Dunia Bw. Holger Krag akifafanua jambo kwa ujumbe wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇