Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari, kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam, kuhusu mafanikio ya benki hiyo.
Na Richard Mwaikenda
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari, kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Baadhi ya watendaji wa CRDB wakiwa katika mkutano huo
Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakisikiliza kwa makini wa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo akielezea kuhusu mafanikio ya benki hiyo
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa akiruhusu wanahabari kuuliza maswali kwa MD Nsekela wakati wa mkutano huo..
MD Nsekela akipongezwa na wafanyakazi baada ya kumaliza kuzungumza na wanahabari kuhusu utendaji mzuri wa benki hiyo.
Na Richard Mwaikenda
BENKI ya CRDB imefanikiwa
kupata faida kubwa ya Bil. 92 baada ya kodi
kwa kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu.
Mafanikio hayo yametangazwa
leo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela katika mkutano na
waandishi wa habari, kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Nsekela amesema kuwa hayo ni
mafanikio makubwa ambayo ni sawa na asilimia 76 na kwamba kwa kipindi kama hicho mwaka jana, walipata
faida sh. Bil. 52.
Ametaja siri ya mafanikio
hayo kuwa ni kuwa ni ufanisi , utendaji na uwajibikaji wa imu nzima ya
wafanyakazi, kuwa karibu na wateja ambao amana zao hadi sasa imefikia Sh.
Trilioni 4.8 hivyo kuongoza mabenki mengineTanzania.
Alitaja zingine kuwa ni;
kuwajali wateja, kuboresha huduma na kuongeza wigo wa kutoa mikopo kwa wateja
yenye riba nafuu zinazoanzia asilimia
14.5, 15, 17, na 18 hali inayochochea wateja wengi kujiunga na benki hiyo.
Nsekela amesema kuwa jambo
lingine linaloifanya benki hiyo kuzidi kuwa kinara nchini ni kuwajali wateja kwa kuwasogezea huduma kwa
kusajili mawakala ambapo hadi sasa benki hiyo ina mawakala 11,612 nchi nzima. Ina matawi 240, ATM 551, na vituo vya mauzo (POS),2400 2400
Jambo lingine alilolitaja
kuwa linaongeza ufanisi wa benki hiyo ni ubunifu, kwani hivi karibuni
ameanzisha dawati maalumu la kuwa hudumia wanawake kwa kuwapatia mikopo yenye
masharti nafuu ikiwemo kuwaidhinishia mikopo bila kuwa na dhamana, wakitambua
wengi wao hawana dhamana.
Pia masuala ya dijitali
yamechangia kwa aslimia kubwa wateja kuwa karibu na benki hiyo kwani
hujihudumia popote walipo kwa kutoa fedha kupitia simu banking kwa kutumia
mitandao mbalimbali ya simu.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari, kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Baadhi ya watendaji wa CRDB wakiwa katika mkutano huo
Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakisikiliza kwa makini wa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo akielezea kuhusu mafanikio ya benki hiyo
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa akiruhusu wanahabari kuuliza maswali kwa MD Nsekela wakati wa mkutano huo..
MD Nsekela akipongezwa na wafanyakazi baada ya kumaliza kuzungumza na wanahabari kuhusu utendaji mzuri wa benki hiyo.
Vizur
ReplyDelete