LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 15, 2019

BODI YA UTALII YAGAWA VIPEPERUSHI VYA MAONESHO YA SITE 2019, JIJINI DAR




Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Jaji Maiko Mihayo akiwa anagawa vipeperushi vya matangazo ya Maonesho ya Ya tano ya Swahili International Tourism Expo (SITE) kwa wananchi wanaopita na magari kwenye Barabara ya Kenyata, Maonesho hayo yanatarajia kuanza Oktoba 18-20 mwaka huu kwenye Viwanja vya Mlimani City.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Jaji Maiko Mihayo akiwa anamuangalia muuza magazeti aliyemkabidhi vipeperushi na kuviweka ndani ya magazeti na kuwapatia wateja wake. Zoezi hilo la kugawa vipeperushi limefanyika  leo kwenye barabara ya Kenyata.

 Afisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB), Godfrey Tengeneza akigawa vipeperushi vya matangazo ya maonesho ya tano ya Swahili International Tourism Expo (SITE) yanayotarajia kuanza Oktoba 18-20 mwaka huu kwenye Viwanja vya Mlimani City.
Mratibu wa Onesho la SITE 2019Joseph Sendwa akigawa vipeperushi vya matangazo ya maonesho ya tano ya Swahili International Tourism Expo (SITE) yanayotarajia kuanza Oktoba 18-20 mwaka huu kwenye Viwanja vya Mlimani City.

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Jaji Mstaafu Frank Mihayo amefanya zoezi la kugawa vipeperushi kwa ajili ya maonesho ya tano ya utalii ya Swahili International Tourism Expo (SITE).

Maonesho hayo yanatarajia kuanza Oktoba 18-20 ya mwaka huu katika Viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kumaliza zoezi la kugawa vipeperushi hivyo kwa wananchi, Jaji Mihayo amesema wataendelea na zoezi la kugawa vipeperushi katika maeneo tofauti hadi kufikia siku ya maonesho hayo.

Amesema, watanzania lazima wafahamu umuhimu wa maonesho haya ambapo wageni zaidi ya 400 kutoka mataifa mbalimbali watakaonesha mazao ya utalii wa aina tofauti.

"Watakuja watalii wengi sana, maana kila balozi zetu zimefanikisha kuwaleta wadau wa utalii na wataonesha mazao mbalimbali ili kuhakikisha onesho linafanikiwa,"amesema Mihayo.

Mihayo amesema, matayarisho yamefikia hatua nzuri, kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa ngoma zetu za asili zikiburudisha kusindikiza onesho letu la mazao ya utalii.

"Tunahitaji watu wafahamu bodi ya utalii inafanya nini ili kukuza utalii, na lengo pia ni kuwakutanisha wadau wa utalii mbalimbali wakija kuuza na kununua mazo ya utalii na huu ndio mida mzuri wa wadau wa utalii kuja kuonesha bidhaa zao," amesema

Naye Afisa Uhusiano wa TTB, Godfrey Tengeneza amesema maonesho hayo yatakuwa ya siku tatu na yatafunguliwa Oktoba 18 na kufungwa Oktoba 20 mwaka huu, ambapo maandalizi yamekamilika kwa hatua kubwa .

"Tumeandaa matangazo mbalimbali ambapo yamebandikwa kwenye maeneo tofauti,  na tumejiandaa kwa kiasi cha kutosha na nawaomba watanzania waje kutembelea na kujiona mazao ya utalii kutoka dunia nzima,"amesema Tengeneza.

Pia, kutakuwa na semina kutoka kwa wataalamu waliobobea kwenye masuala ya utalii.

Bodi ya Utalii inafanya onesho lake tano la  Utalii la Kimataifa nchini (SITE) linatarajiwa kukutanisha wadau wa utalii wa Kimataifa wa ndani  ya nchi zaidi ya 400.

Washiriki wa maonesho hayo ni mawakala wa utalii wa Kimataifa, waandishi wa habari za utalii wa kimataifa na wafanyabiashsra wa utalii kutoka Tanzania na nchi za jirani.

Washiriki hao wanatarajiwa kutoka nchi zaidi ya 57 Ulimwenguni na  baadhi ya nchi mashuhuri zinazotarajiwa kuleta washiriki ni Marekani, Uingereza, Italia, Ujerumani, Urusi, China, Sweden, Afrika Kusini, Seychelles, Mauritius, Rwanda, Malaysia, Kenya, Thailand, India, Korea ya Kusini na Singapore.

Maonesho hayo yamekuwa na mafanikio makubwa kwani mwaka 2014 kampuni za uoneshaji utalii zilikuwa 40 na mwaka 2018 zimekuwa 152 na wadau wa safari wakubwa wa kimataifa kwa mwaka 2014 walikuwa 24 na mwaka 2018 walikuwa 335.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages