Mmoja kati ya wananchi walioshiriki kumuua mbwa huyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera mh. Hashimu Murshid Ngeze akizungumza jambo na waandishi wa habari (pichani hawapo) kuhusu kichaa cha mbwa |
Na Lydia Lugakila Bukoba
Wananchi katika kata ya katoro Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wamefanikiwa kumuua Mbwa aliyedaiwa kuwa na kichaa na kusababisha kuwajeruhi kwa kuwang’ata wananchi 18 katika hiyo.
Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 8, 2019 na Afisa mtendaji wa kata ya katoro katika Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani kagera Innocent Mzungu ambaye ametaja mbwa huyo kuwa kero katika kata hiyo kwa kuwang’ata wananchi 18 na kusababisha watoto na watu wazima kuamua kujifungia ndani masaa yote huku wanafunzi wakishindwa kwenda shule ili kukwepa madahara hayo.
Katika taarifa hiyo mzungu amesema kuwa mbwa huyo alifanya madhara hayo kati ya Septemba 5 na 6 mwaka huu na kufanya idadi hiyo kuwa 18.
Mtendaji huyo amesema kutokana na kero hiyo yenye madhara makubwa ndipo wananchi wa kijiji cha Ruhoko wamefanikiwa kumuua mbwa huyo na kutolewa tamko kwa kila mwananchi aliyefuga mbwa na paka kuwapeleka wanyama hao kupatiwa chanjo Sepemba 9 mwaka huu watakaokiuka tamko hilo kutozwa faini.
Mwandishi wa habari hii Hakuishia hapo amefanikiwa kumtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera mh. Hashimu Murshid Ngeze ili kujua hatima ya tukio hilo ambapo amesema kuwa Kipindi cha mwezi jana tukio hilo liliikumba kata ya Rukoma
wilayani humo ambapo baadhi ya wananchi waling’atwa na mbwa mwenye kichaa jambo liliwafanya viongozi hao kukaa kwa maana ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo pamoja na mkuu wa idara ya mifugo na kukubaliana kwa pamoja kuwa mbwa ambao wanabainika kuwa na kichaa wachanjwe na kuwa hivi karibuni madawa ya kuchanja yaliletwa na tayari zoezi la kuchanjwa kwa mbwa hao linaendelea ndani ya wilaya hiyo
‘’Mwaka 2018 mbwa baadhi walichanjwa lakini wananchi akiwemo wafugaji wenyewe walikaidi kupeleka mifugo hiyo kupata chanjo natoa agizo kila mbwa achanjwe’’ amesema,
Ametoa wito kwa wananchi wanaofuga mbwa kuhakikisha wale ambao wanasadikika kuwa na kichaa wafungiwe ndani wakati zoezi la kuwachanja likiendelea
Katika hilo amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanashirikiana na wananchi ili kufanikisha zoezi hilo na kuwa ni agizo la lazima kila mbwa kupatiwa chanjo ili kuepusha madhara katika jamii.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇