LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 15, 2019

WABUNGE UINGEREZA: BORIS JOHNSON ATOE JIBU KALI KWA AHADI ZA KIVAMIZI ZA NETANYAHU

Katika barua hiyo iliyoandikwa Jumamosi ya jana kwenye tovuti ya kitivo cha Mahusiano ya Uingereza na nchi za Kiarabu, wabunge hao wamesisitiza kwamba serikali ya London na washirika wa Ulaya ni lazima waifahamishe Israel kwamba kitendo cha kukiuka sheria za kimataifa, kitakua na hatma mbaya kwenye mahusiano kati yao na Israel. Aidha barua hiyo imebainisha kwamba ahadi za Benjamin Netanyahu za kuyaunganisha baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Israel, zinatishia usalama wa eneo na kuongeza kwamba, Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza ni lazima aitambue Palestina kupitia mipaka iliyoainishwa mwaka 1967.
Benjamin Netanyahhu, Waziri Mkuu wa Israel anayekosolewa kila mahali
Jumanne iliyopita, Waziri Mkuu wa utawala katili wa Kizayuni na katika kampeni za uchaguzi wa bunge ambao umepangwa kufanyika siku ya Jumanne, alitoa ahadi kwamba iwapo ataibuka mshindi katika uchaguzi huo, basi atayaunganisha baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi zingine za Wapalestina inazozikalia kwa mabavu. Kufuatia matamshi hayo, nchi nyingi za dunia na asazi za kimataifa, zimeyataja matamshi hayo ya Netanyahu kuwa ni ya kibaguzi na yanayokiuka sheria za kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages