Imeelezwa kuwa ili vijana waweze kufanikiwa basi wanatakiwa kuwa na mambo matatu ambayo ni bidii na kujituma mbili kuaminika pamoja na kuheshimika.
Hayo yameelezwa Wilayani Mkuranga mkoa Pwani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) CCM Livingstone Lusinde 'Kibajaj' ambaye pia ni Mbunge wa Mtera wakati wa uzinduzi wa mkuranga ya kijani uliandalia na uvccm wa wilaya hiyo.
Lusinde amesema vijana wanapaswa kuhakikisha wanaaminika na kuheshimika kwa jamii na viongozi kwa ujumla kwa sababu wao ndio tegemeo.
"Naomba niwaambie sio kila kijana anafaa kuwa kiongozi hapana kunamaeneo yanapaswa kuongozwa na watu wazima kwa sababu ya busara zao na vijana tuwe wa kwanza kuwaunga mkono" amesema
Aidha ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawalea watoto wao kwenye maadili ya dini na kuijua ili jamii iwe na kizazi chenye maadili.
"tunataka umoja wa vijana CCM uwekimbilio la watu panapo tokea matatizo na kusaidia jamii panapotokea matatizo, watu wasiporwe, wasiibiwe mtoe taarifa polisi tunataka muwe mfano katika jamii."amesema
Hata hivyo ameongeza kuwa wanataka vijana wa CCM wawe wenye heshima kwa wazee wao,kuridhika na nafasi walizonazo sasa na waache tamaa.
kwa upande wake mbunge wa mkuranga Abdallah Ulega amewapongeza vijana hao kwa uzinduzi wa huo na ametoa jezi pamoja na mipira kwa kata saba za wilaya hiyo ambazo ni Kisegese,Bupu,Mbezi,Panzuo,Beta, Njianne na Kitomondo.
Ulega amesema jenzi na mipira hiyo aliyotoa kwa ajili ya vijana wa Ccm wilaya ya mkuranga sio kwa kata hizo saba tu bali kwa kata zote 25 za wilaya hiyo.
Hata hivyo amewatoa hafu vijana kuhusiana na Ulega cup na kuwambia kuwa mwaka huu ipo na karibuni itaanza hivyo wao wajiandae.
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuijenga muondombuni mbalimbali na kuiongoza nchi ambayo inajulikana nchini na Duniani kote.
"sisi vijana wa mkoa wa Pwani tunamkubali na kumuunga mkono Rais kwa mambo makubwa anayoyafanya tangu taifa lilipopata uhuru wake Mwaka 1961 "alisema Mlao
Mbunge wa Mtera ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde 'Kibajaj' akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la umoja wa UVCCM wilaya Mkuranga,Ally Mohammed Mbwera baada ya kuwasili leo wilaya ya Mkuranga.(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mbunge wa Mtera ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde 'Kibajaj' akihutubia katika uzinduzi wa tamasha la Mkuranga ya Kijani lililofanyika leo katika viwanja vya (CCM) wilaya ya Mkuranga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, (Mb) wa Mkuranga,Abdallah Ulega akisalimiana na Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao baada ya kuwasili katika tamasha la Mkuranga ya Kijani lililofanyika leo katika viwanja vya (CCM)
Kijana wa Chipukizi wa wilaya ya Mkuranga akimvika Skafu Mbunge wa Mtera ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde 'Kibajaj' mara baada ya kuwasili Ofisi ya CCM kuzindua Tamasha la Mkuranga ya Kijani lililofanyika leo katika viwanja vya (CCM) wilaya ya Mkuranga.
Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao akizungumza katika uzinduzi wa tamasha la Mkuranga ya Kijani lililofanyika leo katika viwanja vya (CCM)
Mbunge wa Mtera ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM Livingstone Lusinde 'Kibajaj' akisalimiana na Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, (Mb) wa Mkuranga,Abdallah Ulega (katikati) akizungumza katika tamasha la Mkuranga ya Kijani lililofanyika leo katika viwanja vya (CCM)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,(Mb)wa Mkuranga,Abdallah Ulega (katikati) kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega. wakiserebuka
Wana CCM wakiserebuka
Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega (kuali)
Wana CCM wakiserebuka
Wana CCM wa Wialaya ya Mkuranga wakiserebuka.(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇