LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 25, 2019

SERIKALI YA CHINA: MAREKANI IACHE KUICHAFUA NCHI HII

Geng Shuang ameyasema hayo katika kikao na waandishi wa habari mjini Beijing akijibu tuhuma za serikali ya Washington kwamba China inakiuka uhuru wa jamii za wachache ndani ya nchi hiyo. Akifafanua suala hilo Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema kuwa, serikali ya Beijing inatetea uhuru wa kidini wa raia wake kwa mujibu wa sheria. Kadhalika Geng Shuang ameongeza kwamba taarifa zilizotolewa na kituo cha utafiti cha Pew Research Center na Gallup, zinaonyesha kwamba, asilimia 75 ya Waislamu nchini Marekani wanaamini kuwepo ubaguzi wa hali ya juu katika jamii ya nchi hiyo dhidi yao.
Geng Shuang, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China
Hayo yamejiri baada ya hivi karibuni Mike Pence, Makamu wa Rais nchini Marekani kutoa madai ya kukosoa hali mbaya ya uhuru wa kidini katika baadhi ya nchi ikiwemo China. Hii ni katika hali ambayo ripoti za uchunguzi nchini Marekani zinaonyesha kuwepo kiwango cha juu cha ubaguzi kuwalenga Waislamu, hasa baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages