Katika kuelekea Msimu wa Ununuzi wa Zao la Korosho 2019/2020 Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amezitaka taasisi za kibenki
kuhakikisha zinawafiki na kuwafungulia akaunti wakulima wa zao la
korosho kutokana na kuondokana na utaratibu wa kuwalipa wakulima
mkononi.
Byakanwa ameyasema hayo mara baada ya kufungua Tawi la benki ya TPB
lililopo Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ambalo limeweza kutoa mikopo
zaidi ya shilingi Bilion Nne mpaka sasa na kuwafikia wakulima wa korosho
zaidi ya 2500 kwa mwaka huu pekee
Akiongea mbele ya wateja pamoja na wananchii waliohudhulia hafla hiyo
Byakanwa ametumia nafasi hiyo kuzitaka taasisi za kibenki zilizopo
katika mkoa wa Mtwara kuhakikisha zinawafikia wakulima wa korosho hasa
katika maeneo ya vijijini.
“Ninazitaka benki zote kuhakikisha zinawafikia wakulima wote wa korosho
kwa sababu hatutakuwa na utamaduni wa kumlipa mkulima mkononi lakini
pia tumeondokana na utaratibu wa mkulima mmoja kupokea malipo ya
wakulima zaidi ya watano wale ambao hawajafungua akaunti kwa hiyo
niiombe TPB kuiona hiyo kama fursa”amesema Byakanwa
Aidha Byakanwa ameongeza kuwa anafarijika kuona huduma nzuri za benki
hiyo kutokana na kutopata malalamiko yoyote kutoka kwa wakulima hasa wa
zao la Korosho.
“Ninafarijika na ubora mnazozitoa huduma mnazozitoa kwa wakulima wetu
kwa mwaka wa pili huu sijapata malalamiko yoyote ya mkulima yoyote
kuhusina na benki ya TPB sio masasi sio Mtwara”
Sabasaba Moshingi ni Mtendaji Mkuu wa benki hiyo anasema kuwa TPB tayari
imeongeza idadi ya matawi hapa Nchini kutoka 32 na kufikisha 77 ambayo
yameweza kuongeza idadai ajira pamoja na kutoa huduma za kifedha kwa
Jamii husika.
“Benki imeendelea kutoa gawiwo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo na
mwaka huu kutokana na faida ya mwaka jana tumeweza kutoa gawiwo la
shilingi Bilioni moja na million mia mbili kwa wanahisa wake ambao
mwanahisa mkubwa ni serikali lakini tumeweza kuongeza idadi ya matawi na
hili la masaSI ni miongoni ya matawi mapya ambayo tunafungua”Amesema
Moshingi.
5733.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akifungua Tawi jipya la
benki ya TPB lililopo wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara ambalo tayari
limeweza kuwafiki wakulima wa zao la korosho zaidi ya 2500,kusoto kwake
ni mtendaji mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshingi.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akikata utepe kuashiria
ufunguzi wa tawi la Benki ya TPB Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara ambalo
Tayari limetoa mikopo ya zaidi ya shilingi billion Nne kwa wakulima wa
zao la Korosho Wilayani hapo.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akiongozana na Mtendaji mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi mara baada ya kutembelea na kukagua huduma mbalimbali zinazopatikana katika tawi jipya la benki hiyo iliyopo Wilaya ya Masasi,Mtwara.
Kikundi cha Ngoma Mchema Group kutoka wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara kikitumbuiza ngoma za kitamaduni za kabila la Wamakua katika uzinduzi wa Tawi la Benki ya TPB Masasi Mkoani Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa mtwara Gelasius Byakanwa akiwa katika Picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa benki ya TPB mara baada ya kufanya ufunguzi wa tawi la benki hilo wilya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akiwa amebeba mtoto wa mmoja wa wananchi walioshiriki katika uzinduzi wa tawi la Benki ya TPB lililopo Masasi Mkoa wa Mtwara,kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TPB Sabasaba Moshingi.
Saidi Mbito kulia akiwa na Sulpis Likanda wakiwa na zawadi ya Ngao waliopewa na Benki ya TPB kama moja ya shukurani kwa kufanya kazi muda mrefu na benki hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇