NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani
(CCM) akizungumza wakati wa ziara yake kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi
Geofrey Hilly kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
WAZIRI
wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)
kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi
Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake wilayani humo katika aliyevaa kofia
ya kijani ni Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu
NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)
kushoto akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini wakati
wa ziara yake leo
NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani
(CCM) kushoto akiangalia chanzo cha maji cha Mto Pangani kilichopo eneo
la Mandera wilayani Korogwe wakati wa ziara yake ya kukagua chanzo
hicho leo
NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani
(CCM) kulia akitembelea kwenye maeneo mbalimbali kwenye chanzo hicho
akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Mary Chatanda wakati wa
ziara yake.
NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani
(CCM) kulia akikagua kwenye maeneo mbalimbali kwenye chanzo hicho akiwa
na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Mary Chatanda kushoto wakati
wa ziara yake.
NAIBU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani
(CCM) katikati aliyevaa koti akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe
Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM)
Mary Chatanda wakati wa ziara yake wakiangalia chanzo cha maji
Chanzo cha Maji cha Mto Pangani ambaho kitatumika kwenye miradi hiyo ya maji
SERIKALI
imesema kwamba itatumia chanzo cha Mto Pangani kutatua tatizo la maji
kwenye miji ya Handeni, Pangani, Muheza na Korogwe ili kuondosha kero
hiyo ambayo imedumu kwa muda mrefu kwenye maeneo hayo
Hatua
hiyo imekuja baada ya serikali kupata fedha dola milioni 500 kutoka
Serikali ya India kuweza kutekeleza miradi wa maji kwenye miji 28 hapa
nchini ambapo zaidi ya wananchi 600,000 watanufaika
Hayo
yalisemwa leo na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati alipofanya
ziara yake kwenye wilaya za Muheza na Korogwe kukagua chanzo maji cha
Mandera ambacho kitatumika kuchukua maji katika mradi mkubwa wa
ukarabati wa mradi wa HTM kwa ufadhili wa fedha za india kwa miji
minne.
Alisema
kwamba kutokana na hilo changamoto ya aji kwenye miji hiyo itakuwa
imepata ufumbuzi kutokana na juhudi kubwa ambazo zimefanywa na serikali
kuweza kupatikana fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.
“Labda
niwaambie kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli
imedhamiria kumaliza changamoto ya maji kwenye mji wa Muheza na maeneo
mengine kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani “Alisema Naibu Waziri
Aweso.
Alisema
kwamba wakati wa utekelezaji wa mradi wa kutoka Maji Mto Pangani kwenye
miji hiyo matenki makubwa na eneo la kutibu maji yatajengewa eneo la
Segera na baadae kupelekea maeneo husika kwa ajili ya wananchi kupata
huduma hiyo muhimu.
“Lakini
chanzo hicho kitakuwa ni cha mserereko kuhakikisha wanapunguza gharama
za uendeshaji wa mradi huo hivyo ni imani yangu kwamba mradi huo
utakapokamilika wananchi wataondokana na adha ya maji kwa dhani ya Rais
kumtua mama ndoo kichwani “Alisema
Hata
hivyo alisema kwamba wahandisi wa Halmashauri wamekwisha kupita maeneo
yote na hivyo hivi sasa wanasubiri kibali kitakapotoka mradi huo utaanza
mara moja ikiwemo kutangaza tenda kuwapata wakandarasi ili mradi huo
uanze kwa wakati.
“Labda
niwaambieni kwamba sisi kama viongozi wa wizara hatutakuwa kikwazo
kuhakikisha mradi huo unaanza kutekelezwa kwa wakati kuwawezesha ananchi
waweze kupata maji”Alisema
Naibu
Waziri huyo alisema kwamba wanatambua uwepo wa changamoto kubwa ya maji
wilaya ya Muheza lakini mradi wa maji utakaotokaa Pongwe utasaidia
kupunguza adha hiyo lakini mradi huo mkubwa utapunguza tatizo la maji.
Awali
akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi
Adadi Rajabu alisema ujio wa ziara ya Naibu Waziri huyo ni ishara kwamba
wilaya ya Muheza inakaribia kufurika maji kutokana na uwepo wa chanzo
hicho kikubwa cha Mto Pangani.
“Naamini
Kata nyingi zitanufaika hivyo niombe wakandarasi waje mapema kazi hiyo
ianze haraka kwa sababu wananchi muheza wamevumilia muda mrefu na kuna
kilio cha tatizo hilo hivyo kupitia mradi huo wanaweza kuondokana na
adha hiyo “Alisema Mbunge Balozi Adadi.
Awali
akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji Mtendaji wa Mamlaka
ya Maji na Usafi wa Mazingira (HTM) Mhandisi Yohana Mgaza alisema
kwamba chanzo cha Mandera hicho kitatumika kuchukua maji kwenye mradi
mkubwa wa ukarabati wa mradi huo wa HTM kwa ufadhili wa fedha za India
kwa miji hiyo.
Alitaja
miji hiyo kuwa ni Korogwe, Handeni,Pangani na Muheza na vijiji
vitakavyokuwa pembeni ya bomba ambapo mradi huo ni mkubwa na utanufaisha
watu zaidia ya laki sita.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇