LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 10, 2019

RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA ASKOFU MKUU JIMBO KUU KATOLIKI KATIKA TAASISI YA MIFUPA MOI

  Rais magufuli jioni ya leo Septemba 10, 2019 amtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi anaendelea kupatiwa matibabu katika Taasisi ya Mifupa MOI.

Rais Magufuli alisema mimi na wasaisizi wangu wote na watanzania kwa ujumla tunakuombea kwa Mungu upone haraka ili uendelee na kazi zako na kuwashukuru madaktari na wauguzi wa KCMC na MOI na kuahidi kutoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1.5.  


Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam nchini Tanzania, Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi amefanyiwa upasuaji wa dharura katika Taasisi ya mifupa (MOI).

Taarifa iliyotolewa na leo Jumanne Septemba 10, 2019 na Kitengo cha Mawasiliamo MOI inaeleza Askofu Ruwa'ichi alipokelewa hospitalini hapo jana Jumatatu saa 5 usiku akitokea Hospitali ya KCMC, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Baada ya kupokelewa hospitalini hapo, wataalamu wa MOI walimfanyia uchunguzi na vipimo na kubaini alihitaji upasuaji wa dharura.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages