Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanzakushoto)akikabidhi kitabu chenye orodha ya minara iliyojengwa na Mfuko waMawasiliano
kwa Wote kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibondo, Ayubu Sebabili, akiwa
ziarani Kigoma. Anayeshuhudia wa kwanza kulia ni Justina Mashiba, Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza
kulia) akimsikiliza kwa makini Justina Mashiba (wa kwanza kushoto),
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, akitoa maelezo
kuhusu mnara wa Itaba wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa
huduma za mawasiliano, Kigoma.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza
kulia) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano
kwa Wote, Justina Mashiba ((wa kwanza kushoto) ya kuhakikisha kuwa
mnara wa Itaba, unawaka muda wote ili wananchi wapate mawasiliano, akiwa
ziarani Kigoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye
(aliyesimama)akihamasisha
wananchi wa Kijiji cha Kigina kusajili laini za simu zao za mkononi
wakati wa ziara yake mkoani Kigoma ya kukagua upatikanaji wa huduma za
mawasiliano.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye
(anayetembea mbele) akitoka kukagua mnara wa Itaba akiwa katika ziara
yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani Kigoma.
****************************
Na Prisca Ulomi, Kigoma.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema
kuwa mwananchi hataweza kupiga wala kupigiwa simu kama hajasajili laini
ya simu yake ya mkononi kwa alama za vidole ifikapo tarehe 31 Desemba,
2019.
Nditiye
ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Kigoma kwenye
wakati akihamasisha na kuelimisha wananchi wa Kata ya Ruhita, Kibuye,
Mrufiti, Itaba, Murungu, Rugongwe, Kasulu na Kibondo mjini umuhimu wa
kusajili laini zao za simu za mkononi.
“Serikali
imeamua watanzania wote wasajili laini zao za simu za mkononi kwa
kutumia alama za vidole ili kila anayepiga simu au kupigiwa atambulike
ili kupunguza changamoto zinazojitokeza ili mawasiliano yaweze kuchangia
kikamilifu uchumi wa chi yetu,” amesema Nditiye.
Amefafanua
kuwa Sekta ya Mawasiliano imeshika nafasi ya tatu kwa mwaka 2016/2017
na ya nne kwa mwaka 2017/18 kwa kuchangia pato la taifa kwa kiwango cha
asilimia 13.1 na kuwa kati ya Sekta tano bora zinazochangia pato la
taifa. Serikali ieamua kusimamia kikamiifu Sekta hii ili kuhakikisha
kuwa inadhibiti wizi wa mtandaoni kupitia simu za mkononi, ulaghai,
uchochezi, utapeli a matumizi mengine ya simu za mkononi kwa kuwa kila
mwanachi atakuwa amesajili laini yake ya simu ya mkononi kwa alama ya
kidole.
Amewahamasisha wananchi waishio maeneo mbali mbali mkoani humo wakatialipofanya nao mkutano wa hadhara kuwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu,wataalamu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wakiambatana na kampuni za simu za
mkononi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Polisi na Uhamiaji
watafika maeneo mbali mbali mkoani humo ili kuendesha zoezi la kusajili
laini za simu kwa wananchi wote wanaotumia na kumiliki simu za mkononi.
Amesema kuwa zoezi hili litafanyika kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwawatanzania
halali wanaotambulika na wenye kadi ya NIDA au namba ya utambulisho
kutoka NIDA wanasajili laii zao ili kuepusha kufanya usajili kwa watu
wasiohusika kwa kuwa mkoa wa Kigoma uko mpakani ambapo kuna mwingiliano
wa watu kutoka nchi za jirani.
Naye
Japhet Amos, mkazi wa kijiji cha Kigina kilichopo kata ya Rugongwe,
Kigoma akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake alimuomba Nditiye
kuhakikisha kuwa wananchi wanapata kitambulisho cha NIDA au namba ya
utambulisho kwa wakati ili wasizimiwe simu zao mara baada ya tarehe ya
wisho iliyowekwa na Serikali kufika a kuomba huduma hiyo ya usajili
itolewe bure.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Kanda ya Kati, Antonio Manyandaaliwafahamisha
na kuwatoa hofu wananchi wote nchi nzima kuwa huduma ya kusajili laini
ya simu ya mkononi kwa alama ya kidole ni bure na hakuna mwananchi
yeyote atakayelazimika kulipia gharama hiyo na ametoa wito kwa wananchi
kuiarifu TCRA yenye ofisi zake sehemu mbali mbali nchini kuhusu jambo
hilo endapo mwananchi yeyote atatozwa gharama za kusajili laini yake na
wakala wa kampui yeyote ya simu.
“Usajili wa laini ya simu kwa alama ya vidole ni bure nchi nzima, mwananchi haruhusiwikulipa gharama yeyote kwa ajili ya kusajili laini ya simu,” amesisitiza Manyanda.
Katika hatua nyingine, akiwa ziarani mkoani humo, Nditiye amekagua upatikanaji wamawasiliano kwenye kata ya Kibuye, Murungu, Rugongwe na Itaba na kutembeleaminara inayotoa mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo hayo na kubaini uwepowa mawasiliano wakati wa asubuhi na jioni na kufifia au kukosekana kabisa wakati wausiku ambapo ameiagiza UCSAF kwa kushirikiaa na TCRA na kampuni za simu zenyeminara yake maeneo hayo kuongeza betri za kutosha ili kuapata umeme wa jua wakuendesha minara hiyo kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma za
mawasiliano hata nyakati za usiku.
“Mawasiliano yako chini sana, mtu anapatikana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumina moja jioni, matukio yanatokea usiku hatuna msaada na tuna mtandao mmoja tu waVodacom,” amesema Emil Mfanye, Diwani wa Kata ya Murungu akizungumza kwaniaba ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa Nditiye na wakazi wa kijiji chaKumhasha alipokuwa kwenye ziara yake mkoani humo ya kukagua upatikanaji wahuduma za mawasiliano, kuhamasisha wananchi kusajili laini za simu kwa alama ya
vidole na kutoa elimu ya manufaa ya anwani za makazi na postikodi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇