Mwenyekiti wa kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Kagera Mhe. Winston Kabantega akizungumza jambo na madereva wanawake (pichani hawapo) kuhusu swalazim l kuzijuwa alama za Barabarni mkoani Kagera Septemba 9, 2019.
NA LYDIA LUGAKILA BUKOBA
Mafunzo ya kwanza ya Elimu kwa Wanawake
waendesha vyombo vya moto yamefanyika
kwa mara ya kwanza katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera yakiwa na lengo la
kuwakumbusha wanawake kuzijua sheria na kanuni za usalama barabaran, ili
kuepukana na ajali za barabarani zinazotokana na uzembe kwa madreva hao.
Mafuzo ya darasa hayo ya kwanza kutokea mkoani hapa yamezinduliwa rasmi na Mwenyekiti wa kamati ya usalama
Barabarani mkoa kagera Mh.Winston Kabantega Septemba 9, 2019 ukumbi wa
Linaz uliopo katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Kabantega Akitoa ufafanuzi wa mafunzo hayo
ya awamu ya kwanza kwa akina mama hao walengwa kutoka
manispaa ya Bukoba amesema lengo kubwa la mafuzo hayo ni kuwakumbusha wakina
mama kuzijua, kuzitambua sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali za kila
mara zinazotokana na uzembe wa Madreva na kusababisha watu kupoteza maisha huku
baadhi ya familia kubaki yatima.
Mwenyekiti huo ametaja Mafunzo hayo ya
yatachukua siku tano yamejikita zaidi
katika sheria za usalama
barabarani,alama,huduma ya kwanza, uzimaji wa moto, polisi jamii, uongozaji wa
chombo cha kila siku, sheria za madreva. Amesema kuna makosa yanafanyika barabarani
ni mengi yakiwemo ya kizembe na kwa mtindo huo mafunzo haya
yatasaidia kupambana na ajali za barabarani za kizembe.
Aidha amesema kwa upande wa akina mama wamekuwa hawana
mwitikio wa ushiriki katika mafunzo
mbali mbali ambayo yamekuwa yakitolewa.
‘’Mafunzo haya yatawalenga akina mama
hata wajasiliamali na watumishi wa serikali na Mimi nimekuwa mdau mkubwa sana
katika hili lakini nimeshuhudia mara kwa mara mwitikio wa akina mama ni mdogo
sana ikilinganisha na wanaume lakini ili kujua kuwa tumejipanga kikamilifu
tutakwenda wilaya za Kyerwa Karagwe, Bihalamuro, Muleba, na Geita na hii ni katika
kuwalenga akina mama tu waendesha vyombo
vya moto alisema.
Amewataka wakina mama hao kujenga
mazoea ya kuudhulia mafunzo mbali mbali ili kuepuka ajali ambapo ametaka
mafuzo hayo kuwalenga wanawake wapatao 64.
Amewahimiza akina mama hao Kuchukua tahadhali wawapo
barabarani , Kujali maeneo muhimu ya kuvukia watoto na kutaja kuwa baadhi ya
Madreva Wanaokiuka sheria ni wale ambao wana uzoefu wa miaka kumi barabarani lakini Wameamua kujisahau badala yake wengi
wao wameambulia kuwa walemavu wa kudumu hivyo
amewataka kutumia vizuri barabara kwa
kuondoa akili ya mwendokasi, Kukwepa kuingia.hasara.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇