LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 20, 2019

INDIA YAPELEKA WANAJESHI MILIONI 1 NA 80,000 KASHMIR

Ikiwa ni katika kuendeleza ukandamizaji wake dhidi ya Waislamu wa eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India, serikali ya New Delhi imetuma wanajeshi wengine 180 kuungana na maelfu ya wanajeshi wake wengine katika eneo hilo.
Mtandao wa habari wa "Dawn News" wa Pakistan umeripoti habari hiyo na kusisitiza kuwa, wanajeshi wapya 180 wa India wametumwa katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na nchi hiyo na hivyo kufanya idadi ya wanajeshi wa India walioko Kashmir kufikia milioni 1 na 80 elfu.
Tangu mwezi mmoja uliopita hadi hivi sasa, serikali ya India imezidisha ukandamizaji wake huko Kashmir baada ya kuvunja utawala wa ndani wa eneo hilo la Waislamu, kulizingira kila upande na kutangaza serikali ya kijeshi.
Hivi sasa Waislamu wa eneo hilo wanateseka kwa uhaba wa chakula na mahitaji muhimu hasa ya tiba kutokana na karantini iliyotangazwa na jeshi la India.
Tarehe 5 mwezi uliopita wa Agosti, serikali ya India ilivunja kimabavu utawala wa ndani wa eneo la Kashmir na kuzidisha masaibu ya Waislamu wa eneo hilo. Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, lengo hasa la serikali ya India ni kuwapokonya Waislamu wa Kashmir ardhi zao na kuwapa Wahindu na Mabaniani na mwishowe kuwafukuza kabisa Waislamu hao kama walivyofanyiwa Waislamu wa jamii ya Rohingya, huko Myanmar.
Kwa miaka mingi sasa wananchi wa Kashmir wanahimiza kutekelezwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuitishwa kura ya maoni katika eneo lao hilo ili wananchi hao wajiamulie wenyewe imma kubakia chini ya India au kuwa huru, suala ambalo serikali ya New Delhi imekuwa ikilipinga muda wote huu.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages