Msemaji wa jeshi la ulinzi la Yemen amesema kuwa brigedi tatu za kijeshi za Saudi Arabia zimeangamizwa kikamilifu baada ya askari jeshi wa Yemen huku wakiungwa mkono na makundi ya kujitolea ya wananchi walipotekeleza oparesheni kubwa ya kijeshi katika mkoa mpakani kusini mwa Saudi Arabia.
Akizungumza huko Sana'a mji mkuu wa Yemen mbele ya vyombo vya habari, Brigedia Jenerali Yahya Saree ameitaja oparesheni hiyo kubwa iliyopewa jina la "Ushindi wa Mungu" kuwa ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu Saudi Arabia na baadhi ya watifaki wake kuanzisha vita huko Yemen miaka minne iliyopita. Amesema oparesheni hiyo imewasababishia wavamizi hasara kubwa kwa upande wa zana za kijeshi na kuuawa pia askari adui.
Ameongeza kuwa, oparesheni hiyo aidha imepelekea kuangamizwa kikamilifu brigezi tatu za wanajeshi adui wa Saudia, kutekwa idadi kubwa ya silaha, yakiwemo mamia ya magari ya deraya, kutekwa nyara maelfu ya vikosi adui ambao wengi wao ni mamluki na wanamgambo raia wa Yemen watiifu kwa rais wa zamani wa Yemen aliyetoroka nchi Abd Rabbuh Mansur Hadi ambao Saudia inawafadhili. Si hayo tu, bali mamia zaidi ya wanamgambo hao mamluki wa Saudia wameuawa na kujeruhiwa katika oparesheni hiyo kubwa ya kijeshi mkoani Najran.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇