LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 13, 2019

ASKOFU RWA'ICHI ASHIRIKI IBADA WODINI AKIWA AMEKAA

Hali ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Ruwa’ichi, inaendelea kuimarika baada ya jopo la Madaktri saba wa MOI kuthibitisha na leo ameshiriki Ibada akiwa amekaa.

Askofu Ruwa’ichi alifikishwa MOI akitokea Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu saa tano usiku ambako alifanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo kwa saa tatu.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano MOI, Patrick Mvungi leo Septemba 13, 2019 alisema  kuwa jopo la wataalamu wanafuatilia hali ya Askofu Ruwa’ichi kila baada ya saa moja.

“Kwa sasa Askofu bado yuko ICU, lakini hatumii mashine ya kusaidia kupumua, hii inaonyesha dalili nzuri na pia wataalamu wameanza kumfanyisha mazoezi ya kuanza kusimama, hivyo watu wasiwe na wasiwasi kwa sababu afya yake inaendelea kuimarika siku hadi siku.

“Baada ya mazoezi ya kitandani ataanza mazoezi ya kutembea na baada ya afya yake kuimarika zaidi  atahamishiwa High Depend Word (HDU). Hii wodi ni maalumu kwa ajili ya wagonjwa ambao afya zao zimeimarika, na leo jioni jopo la mdakitari litakaa na kutadhimini hali ya afya ya Askofu Ruwa’ichi” hivyo tuendelee kumuombea afya yake izidi kuimarika zaidi aweze kurejea katika kazi zake za utumishi kuwalea waumini wa Kanisa lake Katoliki  alisema Mvungi.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages