Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Alkhamisi alikutana na kufanya mazungumzo mjini Kuala Lumpur na Mahathir Muhammad Waziri Mkuu wa Malaysia.
Akiwa katika hatua ya tatu ya safari yake katika eneo la mashariki mwa Asia, Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Malaysia akiwemo Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mahathir Muhammad.
Dakta Zarif amewaambia waandishi wa habari kuwa, mazungumzo yake na Mahathir Muhammad, Waziri Mkuu wa Malaysia yalifana na kwamba, walibadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali yakiwemo ya uhusiano wa pande mbili, masuala ya Ulimwengu wa Kiislamu, vikwazo na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Marekani ambazo zinakinzana na sheria.
Aidha Kuala Lumpur na Tehran zimekubaliana juu ya udharura wa kuundwa kamati ya ngazi za juu ya uhusiano wa pande mbili ambayo itakuwa katika kiwango cha mawaziri.
Kamati hiyo inatarajiwa kuundwa kabla ya safari ya Mahathir Muhammad, Waziri Mkuu wa Malaysia hapo Tehran.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, kamati hiyo itashughulika na uhusiano wa pande mbili katika nyanja zote zikiwemo za ushirikiano wa kisiasa, kimataifa, masuala ya uchumi na usalama.
Kabla ya kuwasili huko Malaysia, Dakta Muhammad Javad Zarif alizitembelea pia China na Japan akitokea barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇