LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 24, 2019

WATU 54 WAPOTEZA MAISHA KATIKA MAFURIKO NCHINI SUDAN

Watu wasiopungua 54 wamepoteza maisha kufuatia mvua kubwa na mafuriko nchini Sudan huku watu wengine wengi wakiathiriwa vibaya kote nchini na janga hilo la kimaumbile.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA Jens Laerke , aghalabu ya vifo vimetokana na mapaa  kuezuliwa na watu kunaswa na umeme.
Ameongeza kuwa zaidi ya nyumba elfu 37 zimeharibiwa au kubomoka, na wakati msimu wa mvua unatarajiwa kuendelea hadi mwezi Oktoba, mvua zaidi zimetabiriwa kunyesha huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kutokea mafuriko. Jimbo la White Nile lililopo kusini mwa Sudan limeathiriwa vibaya zaidi na mvua hizo ambapo watu 66,000 wameathiriwa na nyumba 13,000 kuharibiwa au kubomoka.
Kwa ujumla majimbo 15 kati ya 18 kote Sudan yameathiriwa na kwa msingi huo maafisa wa serikali na mashirika ya kutoa misaada yametoa wito wa misaada ya dharura ya kibinadamu inayojumuisha makazi, chakula, huduma za afya na maji ya safi ya kunywa.
Nyumba iliyobomoka kufuatia mvua kali Sudan
Msemaji wa Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA Jens Laerke amesema kuna haja ya kuchukua hatua za kuzuia kuenea magonjwa yatokanayo na maji machafu.
Aidha baadhi ya barabara sasa hazipitiki na vijiji vingi havina mawasiliano hasa katika majimbo ya White Nile, Kassala, Khartoum na Gedaref.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages